Microsoft inatengeneza kompyuta ya bei nafuu inayofunguka kama kitabu


Microsoft inaweza kufufua upya mpango wake wa mwaka 2009 kutengeneza Courier, dhana ya tablet yenye skrini mbili ambayo haijawahi kutengenezwa rasmi. Bidhaa hiyo ilikuwa na inchi saba, skrini mbili na ilitengenezwa kama kitabu.

“[Teknolojia ya Courier] itatathminiwa kwa matumizi katika bidhaa zijazo za Microsoft , lakini hatuna mipango ya kutengeneza kifaa kama hicho kwa sasa,” Microsoft Corporate VP wa Mawasiliano Frank Shaw alisema kuhusu mradi huu wakati wa kufutwa kwake.

Sasa imeripotiwa kuwa microsoft wanatengeneza kifaa kipya, kilichopewa jina la “Andromeda,” ambacho kinaonekana kuwa sawa na Courier. Ni kifaa kinazingatia matumizi ya kalamu na utendaji wa wino wa kidigitali (digital-ink functionality).

Vyanzo ndani ya Windows Central vinadai Andromeda tayari iko katika awamu ya mfano (prototype phase) ambapo haipaswi kushangaza kwa sababu hapo ndipo Courier iliishia.

Mfano huo umeonekana kuwa mdogo kiasi cha kukaa mfukoni kwa urahisi inatumia programu ya Windows Core OS ya Windows 10 na utekelezaji wa CShell kwajili ya kuonyesha. Pia Inasemekana kuwa na uwezo wa simu. Hata hivyo, vyanzo vinasema kwamba utendaji kama wa simu za mkononi sio lengo kuu na hivyo haina lengo la kuwa mbadala wa smartphone.

Badala yake, Microsoft inataka kuunda digital notebook ambayo watu watatumia sawa na kutumia karatasi na kalamu lakini kwa utendaji wa juu zaidi. Kwa hiyo, ni wazi ni mrithi wa mradi wa Courier.

Microsoft haijatangaza rasmi mradi huo. Hata hivyo, ikiwa uvumi huu ni sahihi, Andromeda notebook inaweza kutoka mapema mwakani hii inamaanisha kuwa tunaweza kupata habari rasmi hivi karibuni.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA