IntanetiMicrosoft

Microsoft Inaongeza Kipengele cha Kudhibiti Habari za Uongo Kwenye Bing

Microsoft imeingia kwenye kupambana na habari za uongo, na kuongeza “Fact Check” kwenye Bing. Facebook ilitangaza kupambana na taarifa za uongo miezi michache  iliyopita, na Google ikatangaza kufanya hivyo pia. Na sasa, Microsoft inajiunga na utaratibu huu. Na hivi karibuni utaona matunda ya kazi hizi katika matokeo ya utafutaji wa Bing (Bing search results).

Inazidi kuwa vigumu kusema ukweli katika taarifa mbalimbali. Na tuna mtandao wa intaneti ambao unapaswa kulaumiwa kwa jambo hili. Hakika, habari za uongo, stori za kuzusha, na nk zilizaliwa na kuenea kabla ya kuja kwa mtandao, lakini ni mbaya zaidi siku hizi.

Habari za uongo ni Biashara Kubwa

Habari za uongo si jambo jipya, lakini sasa linaenea zaidi kuliko hapo awali. Habari zinaandikwa, zinaenea, na kuendelezwa ili kuathiri maoni ya watu juu ya nchi fulani, wanasiasa, na watu maarufu. Na mfumo mzima ni biashara kubwa.

Baada ya kutazama Facebook na Google wote wakijitahidi kuwasaidia watu kutenganisha ukweli kutoka kwa uongo, Microsoft inaongeza kipengele kipya cha UX kwenye matokeo ya utafutaji wa Bing. Kinaitwa “Fact Check”, itaongeza maelezo ya kuangalia ukweli kwa matokeo ya utafutaji bila mtumiaji kuondoka kwenye Bing.

Bing itaongeza maelezo ambayo yanafaa kwa stori za habari na kurasa za wavuti. Hizi zitaonyesha watumiaji mara moja kuwa madai yamezingatiwa na shirika kama Snopes au Politifact, na kuonyesha ni ipi tathmini yao. Kama ni Kweli, Uongo, au katikati.

SOMA NA HII:  Facebook kufanya utafiti ili kuboresha habari zake

Mada zinazohusiana

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako