Microsoft inajaribu mfumo wa “AI search” kwajili ya picha


Microsoft inajaribu mfumo wa utafutaji picha wa AI katika Photos app yake, kwa mujibu wa ripoti ya Engadget.

Microsoft

Ripoti hiyo imesema kuwa toleo la karibuni la Insider Preview kwajili ya app hiyo lina¬† “search bar” ambayo inawawezesha watumiaji kuandika jina la kitu anachotaka ili kupata picha sahihi.

Google Photos na Apple Photos zina utendaji sawa, iliongeza ripoti ya Engadget.

Mfumo wa Microsoft utatumia algorithm ya kutambua picha ili kutafsiri neno lililoandikwa  na kutambua picha zinazofanana na neno hilo.

Microsoft Photos pia zitaunda albamu iliyopendekezwa kuweka picha zilizochukuliwa “karibu mahali sawa na muda unaoendana” pamoja.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA