Apps za SimuSimu za Mkononi

Mgeni Wetu: Zifahamu App 10 Mpya Za Android

App mpya zinahitaji upendo pia, sawa? Kila siku kuna maelfu ya app yanaongezwa kwenye Google Play store, lakini nyingi zinaishia kutotambuliwa na hazipati heshima zinayostahili. Tumeonyesha katika siku za nyuma kwamba jumuiya hii (Mediahuru) inaweza kugundua app nzuri na kuzipeleka kwenye viwango vipya. Safu yetu ya kila wiki ya Mgeni Wetu inaonyesha apps mpya zilizopakuliwa chini ya mara  100,000. Vinjari app mpya za Android tulizozichagua hapa chini na utujulishe unayoifurahia.

Transformers ? The Last Watch Face

Ufafanuzi: michoro ya kubuni inayovutia hii ni Watch face nzuri. Optimus Prime, Bumblebee, Grimlock, Starscream, na Megatron – pia Decepticons na Dinobot – vyote katika Watch face moja inayovutia.

(Play Store)

Draw Animal

Ufafanuzi: Fuata hatua kujifunza kuchora picha za wanyama zinazovutia! Paka, Mbwa, Panda, Samaki na zaidi! Hatua za kina za kujifunza kuchora.Hakuna haja ya ujuzi wowote, jifundishe hatua kwa hatua. Fuata hatua za kukamilisha kazi zako nzuri!

(Play Store)

Astro – Fast Secure Web Browser and Search


Ufafanuzi: Ni app nyepesi, kivinjari (browser) bora kwajili ya Android. Hakuna kitu kibaya kama uzito kwenye kufunguka , na app hii inajibu matakwa yako yote ya kufunga-haraka ikiwa na vitu vingi ndani yake. Ukiwa na kivinjari cha Astro kwenye kifaa chako cha Android, utakuwa na zana za utafutaji za haraka zaidi kwenye vidole vyako. Nini bora zaidi; Astro Browser ni binafsi kabisa.

SOMA NA HII:  Hizi Ndio Simu 4 Bora kwa Wapenzi wa Muziki

(Play Store)

Storm Radar with NOAA Weather


Ufafanuzi: Fuatilia hali ya hewa kama hujawahi kuona kabla kupitia Storm Radar app kwajili ya Android! Ramani kamili yenye mwingiliano ikiwa na ufafanuzi wa masaa 8 ya nyuma na yajayo, kufuatilia kama kuna dhoruba, na tahadhari za hali ya hewa zinakuwezesha kutazama hali ya hewa inayokuja njia yako.

(Play Store)

GoToMyPC

Ufafanuzi: GoToMyPC inakupa uhuru wa kwenda popote unapotakaa na kuunganishwa moja kwa moja kwenye Mac yako au PC yako. Furahia ufikiaji rahisi kwa faili zako, programu na barua pepe na kuongeza tija yako popote unapoenda. Ili kutumia programu hii ya bure lazima kwanza uwe na usajili wa GoToMyPC.

(Play Store)

Family Dollar


Ufafanuzi:Family Dollar app ni njia rahisi zaidi ya kupata akiba kubwa na kuponi kwajili ya maduka maarufu, vitafunio, bidhaa za afya na urembo, nguo, zawadi, midoli na zaidi.

(Play Store)

Persona 5 IM App


Ufafanuzi: Persona 5 IM App inafanya kila kitu unachotarajia kutoka kwenye app ya SMS, kama kusoma, kutuma, kupokea na kufuta ujumbe, ikiwa na ujumbe wa kukujulisha wakati unapkea ujumbe mpya.

(Play Store)

Textra Emoji – Android Oreo Style

Ufafanuzi: Hii ni *add-on* kwenye app ya ujumbe mfupi- SMS ambayo hutumia emojis za karibuni za Android Oreo. Inatoa  (Unicode 9) 2000+ emojis zote ikiwa ni pamoja na utofauti kwenye simu yoyote ya Android.

SOMA NA HII:  Vitu Muhimu Unavyopaswa Kufahamu Kuhusu App ya Boomplay Music

(Play Store)

A/D Watchface


Ufafanuzi: A / D watchface inasimama badala ya Analog / Digital. Watchface hii inaonyesha saa ya digitali na inakuza vizuri katika mchanganyiko wa saa ya analog / digital.

(Play Store)

Pampers Rewards for Parents and Babies


Ufafanuzi: Jiunge na Pampers Rewards na ufurahia faida zote kutoka kwenye mpango huu. Fanya manunuzi yako ya diaper kuwa tuzo na zawadi kwajili ya familia, mtoto wako mdogo, au mtoto wako aliyezaliwa.

(Play Store)

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako