Sambaza:

App mpya zinahitaji upendo pia, sawa? Kila siku kuna maelfu ya app yanaongezwa kwenye Google Play store, lakini nyingi zinaishia kutotambuliwa na hazipati heshima zinayostahili. Tumeonyesha katika siku za nyuma kwamba jumuiya hii (Mediahuru) inaweza kugundua app nzuri na kuzipeleka kwenye viwango vipya. Safu yetu ya kila wiki ya Mgeni Wetu inaonyesha apps mpya zilizopakuliwa chini ya mara  100,000. Vinjari app mpya za Android tulizozichagua hapa chini na utujulishe unayoifurahia.

Brevent

Brevent

Ufafanuzi: Brevent inaweza kufanya app kusubiri au kuifanya isimame kufanya kazi, kuzuia app kufanya kazi kwa muda mrefu. Haihitaji ROOT, wala kurekebisha mfumo. Zaidi ya hayo, huenda haifanyi kazi vizuri kwenye ROOT au mfumo uliobadilishwa.

adidas All Day 

adidas All Day

Ufafanuzi: Kugundua mazoezi ya kila siku na mazoezi ya yoga, maelekezo ya lishe bora, na njia za kuboresha nguvu zako na akili hii ni app ya kuwa nayo kila siku kutoka adidas. Jenga tabia mpya na kuboresha ustawi wako kwa kutumia  All Day activity tracker. Weka mpango wako wa kufanya kazi na kufuatilia metrics zako ikiwa ni pamoja na kiwango cha kalori kilichoungua, hatua ulizotembea na umbali uliokimbia.

Replaio Radio – Music & Info

Replaio

Ufafanuzi: Replaio ni online radio player ya bure imeunganishwa na vituo zaidi ya 30,000 ulimwenguni kote. Unaweza kusikiliza vituo vya redio vya mtandaoni na vituo vya AM / FM vinavyopatikana mtandaoni, na pia kugundua vituo vipya kwa kutumia kipengele cha “Explore”!

 

SOMA NA HII:  Tecno vs Infinix – Simu Gani ni Nzuri ?

WD2GO Cloud

WD2GO Cloud

Ufafanuzi: App ya simu ya WD2GO inakuwezesha kufikia hifadhi yako ya WD2GO cloud. Kuhifadhi picha kutoka kwenye kifaa chako cha Android. Kutuma na kushirikisha faili zako kwa wengine.

XDA Feed

XDA FeedUfafanuzi: XDA Feed ni moja ya “feed”  bora zaidi kutoka XDA forums, inakuwa updated mara kadhaa kwa siku. Ikiwa ni ROM mpya, kernel, au mod kufanya simu yako kuwa bora, mandhari, wallpaper, au icon pack, ili kuweka vitu sawa, XDA Feed itaendelea kukujulisha vitu vipya kutoka kwenye XDA forums.

GoToAssist (Remote Support) (new)

GoToAssistUfafanuzi: GoToAssist (Remote Support) inakuwezesha haraka na kwa urahisi kutoa msaada kwa desktops na vifaa vya simu kwa kutumia simu yako ya Android au tablet. Wasaidie wateja wako wakati wowote wanaohitaji msaada.

GoToAssist Customer (new)

GoToAssist Customer

Ufafanuzi: GoToAssist (Customer) inaruhusu mawakala wa Remote Support wa GoToAssist kutoa ushirikiano kamili wa skrini, remote control, usaidizi kwa mfumo wa mazungumzo, na ushirikiano wa kamera (live camera streaming kutoka kwenye kifaa chako hadi kwa wakala wako wa msaada) kwa vifaa vya Samsung na LG vinavyoendesha na toleo la Android OS 4.2 na zaidi. Pia hutoa ushirikiano wa skrini kwa vifaa vinavyoendeshwa na Android 5.x (Lollipop) na zaidi.

Changes

Changes

Ufafanuzi: Changes inakuwezesha kufatilia masasisho(updates) ya application na mabadiliko yake.

HTC People

HTC People

Ufafanuzi: HTC People inakupa app kuu ili kukusaidia kusimamia mawasiliano yako, kupiga simu na call logs. Dhibiti mawasiliano yako. Dhibiti data katika vyanzo tofauti. Funga simu unazopigiwa kutoka kwa watumaji wa spam. Unganisha au ondoe anwani zilizojirudia. Ingiza au safirisha(Import au export) mawasiliano kutoka kwenye SIM au hifadhi ya Simu.

Triangle: More Mobile Data

Triangle

Ufafanuzi: Ni data zako, hivyo unapaswa kuwa na udhibiti wa jinsi inavyotumika. Triangle “Data Saver” inakuwezesha kudhibiti apps ambazo hutumia data za simu ili kuzuia matumizi yasiyohitajika ya data. Ruhusu apps maalum kutumia data kwa dakika 10 au 30 kwa muda maalumu, au siku zote.

Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako