Nyingine

MFANYABIASHARA MAARUFU JIJINI MBEYA ASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KUJIUSISHA NA MADAWA YA KULEVYA

JESHI la polisi Mkoani Mbeya, linamshikilia mfanyabiashara maarufu Jijini Mbeya, Steven Samweli (Maranatha), kwa tuhuma za kujihusisha na biashara za dawa za kulevya.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Dhahiri Kidavashari alisema kuwa Maranatha, alikamatwa juzi, kwenye moja ya duka lake la biashara za dawa baridi kwa matumizi ya binadamu.

Alisema, baada ya polisi kupata taarifa za kuhusishwa kwa mfanyabiashara huyo na mtandao wa dawa za kulevya, liliweka mtego na hatimaye kufanikiwa kumtia nguvuni na sasa anahojiwa.

Aidha, kukamatwa kwa mfanyabiashara huyo, kunafikisha idadi ya watu nane wanao tuhumiwa kujihusisha na uingizaji, usambazaji na utumiaji wa dawa za kulevya Mkoa wa Mbeya, huku watumiaji wanaoshikiliwa wakiwa ni 23.

Credit Fahari news

Soma na hizi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Check Also

Close
Close