Habari za Teknolojia

Mfahamu Kijana wa miaka 17 aliyejitengenezea simu

Kijana wa miaka 17 kutoka nchini Canada ambaye alijitengenezea mwenyewe simu baada ya mama yake msomali kusema kuwa hana uwezo wa kumnunulia simu ya smartphone.

Mo Omer anatarajia kuuza zaidi simu alizotengeneza katika mataifa hasa ya Afrika

Mo Omer – ambaye anajiita mwenyewe “tech nerd” – alitengeneza simu ya smartphone kuanzia mwanzo , na anasema ataiuza kwa dola $180.

“Ina kila kitu unachoweza kukipata katika simu ya kawaida, ni kwamba tu haina gharama kubwa ,” ameiambia BBC.

Simu “sio vifaa vigumu kutengeneza”, aliongeza- na akasema ana azma ya kuzipeleka katika baadhi ya maeneo ya Afrika.

“Tumepokea maombi kutoka Nigeria na Algeria na maeneo mengine mengi. Ni soko linalokua kwa kasi ambalo tungependa kuingia “.

SOMA NA HII:  Twitter sasa ina watumiaji milioni 330 kila mwezi

Zinazohusiana

Toa Maoni Hapa:

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako