Nyingine

Meli ya MV. Ruvuma yaingizwa Ziwa Nyasa kwa majaribio Itungi Port, Kyela

Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe, Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria na Mbunge wa Kyela (shati la blue) akishuhudia MV Ruvuma ikitelemshwa majini kwenye cherezo ya bandari ya Itungi, Wilayani Kyela, mkoa wa Mbeya.

Meli ya MV Ruvuma jana Machi 1, 2017 imeingizwa majini kwenye bandari ya  Itungi,Wilayani Kyela mkoani Mbeya.

Zoezi  hilo limeshuhudiwa na Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe, Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria na Mbunge wa Kyela.

Meli hiyo yenye uwezo wa kubeba mzigo zaidi ya tani 1000 inaungana na Meli nyingine mpya MV Njombe yenye uwezo wa kubeba tani kama hizo ambayo iliingizwa majini siku tano zilizopita.

Meli zote mbili zipo kwenye hatua ya mwisho ya utengenezaji na majaribio kabla hazijaanza rasmi kazi ya kubeba mizigo kwenye ziwa Nyasa.

Tayari wateja mbalimbali wamejitokeza kutaka mizigo yao ianze kubebwa na meli hizo mpya, yakiwemo makampuni yanayojishughulisha na biashara ya makaa ya mawe.

Zinazohusiana

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *