Sambaza:

Baada ya wanakijiji kutishiwa na serikali kuwa itabomoa nyumba zao kwa ajili kupisha ujenzi wa barabara mpya, mtu mmoja huko China amelazimika kurudisha nyumba yake nyuma hatua 492 kuepuka kupoteza nyumba hiyo.

Pamoja na serikali kusema italipa fidia kwa wamiliki wa nyumba 165 huko Taixing City, China Jiangsu, mwanakijiji ambaye hakutaka kuachana na nyumba yake ya ghorofa tatu, alitumia 120,000 yuan (£ 13,959) kurudisha nyuma nyumba nzima, kwa kutumia roller za mbao.

Nyumba hiyo imehamishwa kwa muda wa siku mbili tu na zoezi limekamilika tarehe 21 Machi, yeye pia amepewa fidia na serikali kwa ajili ya kusogeza nyumba yake, People’s Daily Online iliripoti.

SOMA NA HII:  Ifahamu Simu ya Tecno S1 na Bei yake Nchini Tanzania

Sambaza:

This article has 1 comment

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako