Home Nyingine Mbowe hajakamatwa, ameenda mwenyewe Polisi- CHADEMA

Mbowe hajakamatwa, ameenda mwenyewe Polisi- CHADEMA

0
0

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe ameenda mwenyewe kwenye kituo cha Polisi, Central jijini Dar es Salaam si kwa kukamatwa, taarifa ya cha hicho imesema hii inakinzana na taarifa zilizosambaa mchana kuwa Mbowe alikamatwa na polisi maeneo ya Mikocheni ambako alienda kujificha ili asikamatwe.

Taarifa ya katibu wa chama hicho mkoa wa Dar es Salaam, H Kilewo imesema:

Waheshimiwa Viongozi na Wanachama wa Chadema Dar es salaam, Siku ya leo Mwenyekiti wa Chama Mhe.Freeman Mbowe akiwa Kwenye Mkoa wetu wa Dar es salaam, Ameamua kwenda Central baada ya kuwepo na Taarifa nyingi kwenye vyombo vya habari na Mitandao ya kijamii kuwa anahitajika nao. Taarifa za kusema ya kwamba jeshi limemkamata na kumpeleka Central ni taarifa za uongo ambazo hatujui zinataka kulenga kitu gani…Taarifa sahihi ni Kwamba Mhe.Freeman Mbowe ameamua kwenda baada ya taarifa kuzagaa kuwa anatafutwa

Siku ya Jumamosi Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro alimpa kiongozi huyo muda wa saa 48 za kujisalimisha vinginevyo watamtafuta kwa njia wanazozijua wao.

Mbowe aliitwa polisi kwaajili ya mahojiano kutokana na tuhuma za kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya pamoja na kulisababishia usumbufu na gharama jeshi la polisi.

(0)

LEAVE YOUR COMMENT

Your email address will not be published. Required fields are marked *