Nyingine

MBEYA KUANZA KUTANGAZA VIVUTIO VYAKE VYA UTALII

Afisa Utalii Jiji la Mbeya, Levina Modest akitoa taarifa ya vivutio vya utalii vinavyopatikana ndani ya Jiji la Mbeya wakati wa kikao cha Wadau wa Utalii. Diwani wa Kata ya Sisimba Jofrey Kajigili akichangia jambo katika Kikao cha wadau wa Utalii katika Jiji la Mbeya. Mwenyekiti wa Wenye Hoteli Mkoa wa Mbeya, Jeremia Mahenge akichangia namna Jiji linavyoweza  kutumia vivutio ilivyonavyo kuingoza kipato Mkufunzi wa Chuo kikuu cha Teofilo Kisanji(TEKU), Frank Haukila akichangia mada katika kikao cha wadau wa Utalii jiji la Mbeya kilichofanyika katika ukumbi wa Elimisha Wadau wa Utalii Jiji la Mbeya wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kikao cha kujadili namna ya kuvitangaza vivutio vya Utalii Jiji la Mbeya.

HALMASHAURI ya Jiji la Mbeya kwa kushirikiana na wadau wa Utalii imeunda kamati ndogo ya wadau 16 ambayo itaainisha na kuvitambua vivutio vya utalii ndani ya Jiji la Mbeya.

Kamati hiyo iliundwa jana katika kikao jumuishi cha wadau wa Utalii jijini Mbeya kilichoandaliwa na Shirika la Elimisha kwa ushirikiano na Mkurugenzi wa Jiji la Mbeya.

Wadau hao walisema Halmashauri ya Jiji la Mbeya inavivutio lakini ilibweteka kuvitangaza.

Awali akifungua kikao hicho, Diwani wa Kata ya Sisimba Geofrey Kajigili (CHADEMA)  alisema Halmashauri ya Jiji halina kitu cha kujivunia kwenye utalii licha ya kuwa na vivutio vingi pamoja na jografia nzuri yenye uoto wa asili ambao unaweza kuendelezwa.

Naye Mkurugenzi wa Elimisha, Festo Sikagonamo alisema lengo la kikao hicho ni kujadili na kuweka mkakati wa pamoja juu ya namna ya kukuza shughuli za utalii jijini Mbeya.

Wakichangia kwenye kikao hicho, walisema Jiji linapaswa kubainisha maeneo yote kisha kuandika maelezo yake kwa kina kabla ya kutangaza.

Walishauri kuundwa kwa kikosi kazi kidogo ambacho kitapitia maeneo yote yenye vivutio kisha kupata historia iliyojitosheleza na kuweka kwenye kumbukumbu kabla ya kutangaza kwa wananchi ili kuwakaribisha kutembelea.

Kwa upande wake Afisa Utalii Jiji la Mbeya Levina Modest alisema halmashauri inamaeneo mengi ya utalii ambayo ni vigumu kupata mapato kutokana na kujificha na mengine kuwa barabarani hivyo wananchi kupita na kuviona kirahisi.

Alisema ili kudhibiti hali hiyo ni vema Halmashauri kwa kushirikiana na wadau wa utalii Jiji la Mbeya wakashirikiana kujenga nyumba ya makumbusho ambayo vitu vingi vya kihistoria vinaweza kupatikana hapo pia ikawa ndiyo lango kuu la kutaka kutembelea vivutio.

Alivitaja baadhi ya vivutio vya utalii ambavyo vinapatikana ndani ya Jiji la Mbeya kuwa ni pamoja na Msitu wa matambiko Iganzo, Safu za Milima ya Mbeya na Mbeya peak,Mnara wa Mwenge wa uhuru,chemchem ya maji moto, makaburi ya mashujaa waliopigana vita ya pili ya dunia na mti wa adhabu.

Alisema vingine ni Uwanja wa vita wa majeshi ya Flerimo, makazi ya jeshi la vita (handaki),mahakama ya kikoloni Lyoto,Shule za kikoloni ambazo ni Iyunga sekondari na Loleza Sekondari, mapango ya kikoloni,mji mkongwe Sokomatola, jukwaa la Mwalimu Nyerere na Makanisa ya Kikoloni ya Katoliki na Anglikana.

Aliwataja wajumbe wa kamati na uwakilishi wao kwenye mabano ambao wataanza kazi Februari 28 mwaka huu kuwa ni Fredy Mduma(Iyunga Sekondari), Saul Mwaipaja (Loleza Sekondari), Jofrey Kajigili (Diwani Sisimba), Mwasote(Diwani Iziwa),Frank Haukila (TEKU),Amos Mwangobola (Tour Operator) na Goba (Tour guide).

Wengine ni Jeremia Mahenge (mwakilishi wenye hoteli),Eunice Mbilinyi (Wkala wa misitu), Esther Macha (mwakilishi wa waandishi wa habari),Venance Matinya(TAJATI),GemaMalekela(Utalii),Kilovecha,Fanuel Sabin  na Kazoba kutoka Jiji  na Debora Mwanyanje (Elimisha).

Soma na hizi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Check Also

Close
Close