Sambaza:

Tumbie umewahi fanya matukio gani ya ajabu wakati unasoma sekondari (True Confessions)

Leo nilikuwa nafikiria jinsi nilivyokuwa msumbufu wakati nasoma sekondari. Nilisoma shule ya serikali inaitwa Malangali Boys ipo mkoani Iringa. Kwa kuwa wali tulikua tunakula mala mbili kwa wiki siku za wali nilikua na mtindo wa kwenda na sahani mbili nachukua ya kwanza kisha kiufundi zaidi narudia tena kuchukua ya pili tulikua tunaita “Paper 2”.

Nilikuwa na matukio mengi sana enzi hizo nakumbuka kuna jamaa tulikua tunakaa nae bweni moja usiku alikuwa na tabia ya kukoloma sana hadi inakuwa kero siku moja mimi na rafiki yangu wakati jamaa amelala tukambeba hivyo hivyo na kitanda chake tukampeleka nje jamaa aliposhituka asubuhi anaona amelela nje akaanza kulia amelogwa daaah ilikuwa burudani sana siku hiyo.

SOMA NA HII:  Orodha ya Maneno ya Teknolojia na Tafsiri zake kwa Kiswahili

Wewe unakumbuka tukio gani la ajabu ulilofanya sekondari. Kumbuka kumwomba Mungu akusamehe matukio yako….mada hii ni kwa lengo la kukumbushana tu maisha yetu enzi tupo shuleni.

Sambaza:

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako