Maswali 8 ya kujiuliza kabla ya kununua programu ya Antivirus


Tunatarajia, unaposoma chapisho hili, tayari una programu ya kupambana na virusi (antivirus) yenye ufanisi na inafanya kazi kwenye komputa yako.

Kama haipo hivyo, natumaini unatambua umuhimu wa kuwa na programu inayosimamia ulinzi na usalama wa kompyuta yako, hata ikiwa ni bidhaa ya bure, kama vile “AVG Free”.

Ikiwa, kwa upande mwingine, unatafuta programu bora ya kupambana na virusi basi ni maswali gani unapaswa kujiuliza?

kununua-programu-ya-Antivirus
1. Je, programu hii ya ANTIVIRUS itakuwa inafanya kazi kwa ufanisi?

Unahitaji kuhakikisha kwamba suluhisho lolote la kupambana na virusi unaloweza kutumia linaweza kukabiliana na vitisho vya hivi karibuni, kama vile mdudu wa Conficker.

Kwa kuzingatia jinsi vidudu na virusi vinavyo sambaa kwa haraka kwenye mtandao, sasisho (updates) za kuchelewa zinaweza kusababisha madhara kwenye ufanisi wa programu ya kupambana na virusi.

Wakati karibu programu zote za anti-virus zinakulinda kwa kupambana na viruses, worms and trojans si zote hutoa ulinzi dhidi ya vitisho vya karibuni, yaani wizi wa utambulisho, ambao hutokea wakati data nyeti zimeibiwa kwenye mtandao wa kuuza vitu mtandaoni na mtandao wa benki.

Ikiwa kiwango hicho cha ziada cha usalama ni muhimu kwako basi unaweza kuwa na bidhaa chache za kuchagua, hata kutoka kwa wauzaji wakuu.

2. Je, programu hii ya ANTIVIRUS ni rahisi kutumia?

Sio kila mtu ni mtaalamu wa kompyuta au mtaalamu wa usalama.

Ni kweli, nimekutana na watu wengi ambao hawajui kufanya kitu kingine kwenye kompyuta zaidi ya kuwasha kompyuta zao!

Ikiwa wewe ni mmoja kati ya watu hao basi hakuna kitu kingine muhimu zaidi ya kuwa na bidhaa ya kupambana na virusi ambayo ni rahisi kutumia.

Kwa mtumiaji mdogo wa kompyuta, vitu muhimu vinaweza kuwa interface rahisi au urahisi wa kuelewa mwongozo wa mtumiaji (user guide).

Urahisi huo katika matumizi haupaswi kupuuzwa na wale ambao hutoa programu za usalama – ikiwa mtumiaji wa wastani ana shida kufunga na kusanidi programu (installing and configuring) yoyote ile basi ufanisi wake huwa duni.

3. Ni kwa jinsi gani inafanya “UPDATES” na inachukua muda gani kutambua virusi vipya?

Kama nilivyosema awali vidudu na virusi hutafutiwa ufafanuzi, ikiwa ni hatua moja mbele ya suluhisho.

Kwa bidhaa ya kupambana na virusi “antivirus” ili kuwa na ufanisi inafaa kuendana na vitisho vya hivi karibuni.

Ikiwa programu ya usalama unayotafuta haina update angalau kila siku basi napenda kupendekeza uachane nayo na kutafuta nyingine ambayo inafanya.

4. Je! programu ya ANTIVIRUS inafanya kazi muda wote?

Ikiwa unachagua bidhaa ambayo hutoa “real-time scanning” basi hiyo ina maana kwamba washambuliaji wabaya (malicious attackers), kama vile “worms na viruses”, wataonekana moja kwa moja wanapojaribu kuingia kwenye mfumo wako.

Hii inamaanisha utapewa ulinzi imara dhidi ya vyanzo vingi vya maambukizi kama vile downloads kutoka kwenye wavuti na email attachments.

Ikiwa bidhaa ya kupambana na virusi haitoi huduma ya kuscan inayoendelea basi kuna kila dalili itatambua na kuchunguza vitisho baada ya kuambukiza mfumo wako na, uwezekano, kuenea kwenye mtandao wako au vifaa vingine.

5. Je, programu hii haikwamishi mfumo wako?

Kwa miaka mingi nimetumia bidhaa mbalimbali kutoka kwa wauzaji wengi ikiwa ni pamoja na McAfee, AVG, Norton na Avast.

Kwa sehemu kubwa, sijawahi ona zikifanya kazi nyuma ya mfumo wangu wa kompyuta.

Hata hivyo, baadhi ya bidhaa ambazo nimetumia na hazijulikani sana zimepunguza ufanyaji kazi wa mfumo wa kompyuta yangu hadi kufikia hatua ambayo niliona hazifai tena, hasa wakati nafanya scan ya drives zangu zote.

Isipokuwa unaweza kupanga ratiba hiyo wakati hautumii kompyuta yako ila hii itaharibu utendaji wako.

Kwa hiyo, napenda kupendekeza kwamba uangalie mtandao ili kuona watu wanasemaje kuhusu bidhaa yako unayoipenda ili kuona matumizi ya programu na malalamiko ya watumiaji.

6. Je, unatakiwa kulipia huduma ya ANTI-VIRUS?

Siku hizi ni muhimu kuuliza kama unatakiwa kulipia programu ya kupambana na virusi.

Wakati bidhaa kama vile AVG Free zina mipaka kwa kulinganisha na ndugu zake wa gharama kubwa zaidi huwa hazina tabia ya kuwa na ufanisi mdogo katika kukabiliana na suala la msingi la kulinda dhidi ya virusi.

Ikiwa wewe ni mtumiaji wa kawaida wa kompyuta na wavuti mtandaoni, basi bidhaa hiyo inaweza kuwa suluhisho kamilifu.

Kwa upande mwingine, ikiwa unatumia kompyuta yako katika taaluma yako, au ni mtumiaji wa benki ya mtandaoni, basi ningependekeza kuwa na programu bora zaidi ya usalama wa mtandao ni mihimu.

(Kumbuka, hata hivyo, kuwa makini na “anti-virus scams” wakati unatafuta ufumbuzi wa bure au nafuu).

7. Inatoa kiwango gani cha msaada wa kiufundi ?

Kiwango cha msaada wa kiufundi inaotoa unafanana na hatua ya # 2 ambayo nimeielezea hapo juu – ikiwa si mtaalam wa kompyuta basi unaweza kuwa na haja ya kuzungumza na mshauri wakati unapokuwa na matatizo au shida na programu.

Kabla ya kumpigia mtoa msaada wa teknolojia unatakiwa kujua –

  • Ni kiasi gani itakugharimu kupiga simu
  • Simu hiyo itajibiwa haraka
  • Je! Fundi ataweza kujibu swali lako kwa njia ambayo utaelewa
  • Je msaada unaopatikana masaa 24 kwa siku

Majibu ya maswali hayo yatakuwa na uzito mkubwa kwa watu wengi juu ya uamuzi wa kununua programu hasa gharama ya msaada ambayo inaweza kufanya hata suluhisho la gharama nafuu inaonekana kuwa ghali sana.

8. Je, kuna toleo la majaribio “TRIAL VERSION” unaloweza kujaribu kabla ya kununua?

Wafanyabiashara wa programu za usalama wenye ubora wanajua kuwa wanatoa bidhaa nzuri na hivyo wanaweza kumudu kutoa majaribio ya bure ya programu zao.

Kwa kawaida, hizi huwa za muda mfupi-au kuwa na vipengele-vichache kwa namna fulani ili kumhimiza mtumiaji kuhamia kwenye toleo kamili la kulipia.

Kwako, hata hivyo, hii ni fursa nzuri ya kujaribu kabla ya kununua na kupata wazo la uhakika wa jinsi programu inavyoendana na matarajio yako, au la.

Je, unachaguaje programu bora ya kujikinga na virusi (antivirus)?

Natumaini pointi nane ambazo nimeziorodhesha hapo juu zimekupa wazo kwamba thamani ya bidhaa yoyote ya kupambana na virusi ni kazi yake zaidi kuliko bei ya awali ya ununuzi.

Je, ni jinsi gani unachagua programu ya antivirus?

Je! Unahitaji taarifa zaidi ili uweze kufanya uamuzi sahihi au unaenda kwa kuzingatia maneno kutoka kwa marafiki au familia.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA