Sambaza:

Masoko ya digitali ni mwavuli unaotumika kuwakilisha masoko yaliyopangwa, kupimwa, na mwingiliano wa bidhaa au huduma kwa kutumia teknolojia ya digitali ili kufikia na kubadilisha wahusika kuwa wateja na kuwahifadhi”. Katika lugha rahisi, masoko ya digitali ni matumizi ya zana zisizo za jadi, za mtandao ili kukuza na kuuza biashara yako.

Masoko ya Digitali

Afrika kwa sasa ipo nyuma ya mabara mengine linapokuja swala la matumizi na kusambaa kwa mtandao wa intaneti, na kutaja masoko ya digitali inaweza kuonekana kama kitu cha kushangaza kwa watu wengi. Lakini mimi ninaomba kutofautiana na wengi.

Kwanza, vyombo vya habari vinaendelea kuwa na ushindani zaidi na zaidi (na gharama kubwa) katika masoko makubwa ya Afrika kwa sababu kuna idadi kubwa ya makampuni ya ndani yanayokua na yanakuja vizuri kwenye soko, na mashirika mengi ya kimataifa pia yanatanua huduma zao katika bara la Afrika . Dar es salaam, Nairobi, Lagos au miji mingine inayoendelea, wajasiriamali wapya watapata shida zaidi kuwekeza kwa njia yenye maana katika kampeni za matangazo kwa njia ya magazeti au TV kujenga bidhaa zao na kupeleka biashara zao kwenye ngazi ya juu.

SOMA NA HII:  Vidokezo 8 rahisi jinsi ya kukuza tukio lako kwenye LinkedIn

Kwa upande mwingine, angalau ikilinganishwa na Magharibi au Asia, asilimia ndogo sana ya makampuni yana mkakati wa masoko ya digitali kwenye shughuli zao, kama vile kuendesha kampeni za matangazo kwenye Google Adwords au Facebook. Nina uzoefu wa kwanza juu ya kuendesha kampeni kwenye masoko kama vile Tanzania na kadhalika ambako gharama za “Cost Per Click” au “Cost Per Mile metrics” ni sehemu tu ya matangazo sawa na Amerika Kaskazini au hata Asia.

Hakika “ubora” wa watembeleji hauwezi kulinganishwa na masoko mengine, lakini maoni yangu ni kwamba kwa mafunzo ya msingi na ujuzi ROI nzuri ipo mbali na kuwa lengo lisilo kuwa rahisi kufikia. Kuna Waafrika wengi zaidi wanaoingia kwenye mtandao, hasa vijana wanaoishi miji, na hakuna njia bora zaidi, kama mjasiliamali, kujenga soko lako na kukuza bidhaa au huduma zako zaidi ya kuzifanya mtandaoni.

SOMA NA HII:  Wanafunzi wa Primary Tanga kuanza kusoma kwa kutumia Tablet

Nitazungumzia zaidi katika machapisho mengine ya baadaye (makala zinazofata) taarifa zaidi kuhusu kampeni maalum za matangazo ambazo zinafanyika mtandaoni ili kutoa picha bora juu ya uzoefu/uelewa wangu binafsi. Nafikiri makampuni mengi zaidi na zaidi yatajihusisha katika soko hili na hii ni moja ya maeneo ambapo faida ya kwanza ni kusonga mbele/kusambaa zaidi kuwa na athari kubwa juu ya kufafanua nani atakuwa juu ya soko ifikapo kesho.

Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako