Utawala nchini Marekani unasema kuwa Korea Kaskazini ilihusika moja kwa moja na kirusi cha wannaCry kilichoadhiri hospitali, biashara na mabenki kote duniani mapema mwaka huu.

Kompiuta zinazotumia Windows zilivamiwa na kirusi hicho na kufungwa ambapo watumiaji walitakiwa kulipa ili kuweza kupata data zao

Kirusi hicho kilidaiwa kuvamia zaidi ya kampuni 300,000 kwenye mataifa 150 na kusababisha hasara ya mabilioni ya dola.

Thomas Bossert ambaye ni msadizi wa Rais Donald Trump, aliyasema haya kupitia jarida la Wall Street Journal.

Hii ndiyo mara ya kwanza Marekani imeilaumu Korea Kaskazimni kwa kirusi hicho.

Ramani inayoonyesha athari ya awali ya WannaCry mwezi Mei 2017

Bw. Bossert anayemshauri Trump katika masuala ya usalama wa ndani wa nchi alisema kuwa madai hayo ni kutokana na ushahidi uliopo.

SOMA NA HII:  Jinsi ya Kugawa Partition Kwenye Windows bila "Kuformat"

Serikali ya Uingereza na kampuni ya kompyuta ya Microsoft waliilaumu Korea Kaskazini kwa kirusi hicho.

Mwezi Mei kompyuta zinazotumia Windows zilivamiwa na kirusi hicho na kufungwa ambapo watumiaji walitakiwa kulipa ili kuweza kupata data zao.

Sambaza:

Written by Mediahuru Team

Hapa Mediahuru, tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi kila siku. - MediahuruDotCom | info@mediahuru.com

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako