Elimu

Orodha ya Maneno ya Teknolojia na Tafsiri zake kwa Kiswahili

on

Teknolojia ya habari na mawasiliano inazidi kutawala maisha yetu ya kila siku na hii inafanya watu wengi wapende kutumia vifaa kama kompyuta na simu za mkononi ili kwenda sawa na ulimwengu wa sasa.

Pamoja na hayo bado kuna ugumu wa kutumia na kufurahia teknolojia hii, achilia mbali athari ambatanishi zinazoweza kusababishwa na kutokuelewa lugha inayotumika ambayo ni kiingereza, pia hata kiswahili chake kinaonekana kuwa kigumu sana kwa watumiaji wapya na hata wale ambao walishazoea kutumia kompyuta kwa kiingereza.

Kama mdau wa TEHAMA nchini bado nina hamu ya kuona Watanzania wenzangu wakuwa huru na kujivunia kutumia kompyuta kwa lugha yao kama wanavyotumia wenzetu.

SOMA NA HII:  Kufikia mwaka huu Magari yote kuanza kutumia umeme

Kuna faida nyingi sana ukijaribu kutathimini hili, hata hivyo ugumu wa kiswahilli chenyewe kinapelekea hata waandaaji wa programu za kompyuta kushindwa kuweka maneno sahihi na marahisi kwenye programu zao.

Mfano neno password ambalo kwa tafsiri halisi ni neno ambalo mtumiaji atatakiwa kuliandika kabla hajapata ruhusa ya kufanya jambo fulani katika mfumo wa kikompyuta limekuwa na tafsiri mbili kinzani ambapo mwisho wa siku mtumiaji ataamua kusema password ni nenosiri, wakati wanazuoni wanasisitiza kuwa password tafsiri yake ni nywila, sasa wangapi kati yetu tulikuwa tunalifahamu neno hili?

Bila kukuchosha, ningependa upakue faili hili na upate kufahamu baadhi ya maneno ya tehama na tafsiri zake. Maneno hayo yanaweza kuwa rejea yako endapo utahitaji kufahamu zaidi neno fulani pindi ukikutana nalo.

Bofya Hapa Kupakua Faili Lenye Orodha ya Maneno Yanayotumika Kwenye Teknolojia

Lengo la mediahuru ni kuelimisha jamii na kuburudisha kwa kutumia teknolojia ya Tehama, Karibu kwenye tovuti hii na usiache kutoa maoni yako kupitia sehemu ya maoni ili kwa pamoja tuzungumze masuala ya teknolojia

About Mediahuru Team

Hapa Mediahuru, tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. Tumejikita kuhakikisha hupitwi na habari yoyote ya teknolojia, endelea kuwa nasi kila siku. - MediahuruDotCom | info@mediahuru.com

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published.