Maneno ya Joh Makini kuhusu picha yake akiwa na Davido

Comment

Joh Makini ameingia kwenye headlines baada ya picha iliyokuwa ikisambaa ikionesha akiwa kwenye maandalizi ya video ya wimbo wake mpya na staa wa Nigeria “Davido”.

Rapper  kutoka kundi la Weusi amethibitisha taarifa za  kuandaa video mpya ya single aliyomshirikisha Davido na kuyaongea haya:

Ni kweli kama mlivyoona kwenye picha mimi niko South Africa kuna video nimekuja kushoot ya wimbo niliofanya na Davido, kwahiyo ni muda mrefu tulikuwa tumepanga kufanya na hatimae jana ndio tumefanikisha na video imefanyika hapa Johannesburg South Africa’-Joh Makini

Up Next

Related Posts

Discussion about this post