Sambaza:

 

Msemaji wa Klabu ya Simba, Haji Manara leo amefungiwa kujihusisha na soka nje na ndani ya mipaka ya nchi ya Tanzania kwa muda wa mwaka mmoja.

Hukumu hiyo imetolewa leo mchana na Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Nchini Tanzania (TFF) pia imemuamuru pia kulipa faini ya shilingi
milioni 9.


Baada ya hilo kutoka, aliyekuwa Msemaji wa Yanga, Jerry Muro ambaye naye Julai mwaka jana alifungiwa kujihusisha na soka kwa mwaka mmoja na kutakiwa kulipa faini ya Sh 3 Milioni, amempa pole hasimu wake huyo na kumkaribisha kijiweni baada ya kulitumikia soka la Tanzania.

SOMA NA HII:  Hali ni mbaya sana kwa tovuti za Pirates na wazee wa Torrent

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Jerry Muro ameandika,

*“Mtuache sasa tupumzike, tuliyofanya kwa taifa hilo haswa kwenye mpira nadhani yametosha, Waswahiba karibu kijiweni @hajismanara

Kamati ya Nidhamu ya TFF ilieleza sababu za kumfungia Muro ni, kukaidi kulipa faini ya Sh 5 Milioni zilizotokana na makosa ya nyuma, kupingana na maamuzi ya TFF kuhusu haki za matangazo ya televisheni na kutumia lugha za uchochezi kabla ya mechi ya Yanga na TP Mazembe

Sambaza:

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako