Sambaza:

Producer kutoka De Fatality Music ambaye ni maarufu kwa kutengeneza nyimbo za Singeli, Mesen Selekta na mkali wa muziki huo “Man Fongo” kwa sasa hawapikiki chungu kimoja.

Selekta ndiye producer wa nyimbo nyingi za Fongo ukiwemo uliompa umaarufu, Hakuna Ushemeji. Kwa mujibu wa Man Fongo sababu za wawili hao kugeuka maadui ni pesa.

Kupitia kipindi cha Twenzetu cha Times FM, Mesen Selekta amesema:

“Ni kweli kuna tofauti ambayo ipo mimi na Man Fongo,”

“Naweza kusema ni kutokuwa na maelewano mazuri kati ya yeye Man Fongo pamoja na studio ya De Fatality kwa ujumla ndio kilichosabisha tofauti,” aliongeza.

Man Fongo amefunguka kuwa kilichosababisha kuvunjika kwa ukaribu wao kuwa ni Mesen alipata deal ya shilingi milioni 10 la Man Fongo kutengeneza tangazo la Tigo lakini akamuambia kuwa ni la milioni 2.5 na kwamba atamlipa laki mbili na nusu na fedha zingine watumie kurekebisha studio yao.

Fongo amesema baada ya kugundua mchezo huo, alikataa kufanya tangazo hilo na kumwacha Mesen njia panda. “Mpaka leo Mesen hataki kuniona hata kunisikia, yaani ananichukia we acha,” alisema Man Fongo.

“Mimi hata kukaa naye kuzungumza naye sitoweza kwasababu kwanza namuona snitch sio mtu mzuri, ina maana milioni 10 yote inatoka anataka kupata hela yeye, ina maana mimi na yeye nani msanii anayeimba?”

“Kataka kutumia yeye, yaani anatumie mgongo wangu mimi nimtengenezee tangazo halafu achukue milioni 10, hivyo ndio tunaishi kweli? Katika milioni 10 mimi nipate laki mbili? Ahh uongo mbali, sio kweli.”

Sambaza:

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako