Mambo Yaliyompa Ushindi Mmiliki wa Facebook Dhidi ya Maseneta wa Marekani


Mmiliki wa Facebook amewaambia maseneta wa Marekani kuwa kampuni yake imekuwa ikipambana na watumiaji wa Warusi wanaotaka kuutumia vibaya mtandao huo wa kijamii.

Bw Zuckerberg alikua akijibu maswali kuhusiana na sakata ya matumizi mabaya ya data za kibinafsi maarufu kama Cambridge Analytica.

Pia amefichua kuwa Robert Mueller, kutoka baraza maalum linalochunguza madai ya Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani wa Mwaka 2016 aliwahoji wafanyakazi wa Facebook.

Bw Zuckerberg amesema kuwa kampuni yake sasa imetengeneza nyenzo za kubaini akaunti gushi. Lakini aliongeza kuwa : “kazi yetu na baraza maalum ni ya siri na ninataka kuhakikisha kwamba katika kikao cha wazi sifichui chochcote juu ya taarifa za siri.

Mark Zuckerberg alijitetea kwa muda wa saa tano katika jopo la wasikilizaji kutoka bunge la seneti la Marekani linalohusika na masuala ya biashara na kamati ya mahakama. Wakati wa hoja dhidi yake, Bw Zuckerberg pia alisema:

  • “Ni wazi sasa kwamba hatukufanya juhusi za kutosha kulinda nyenzo zetu dhidi yakutumiwa kwa madhara”
  • “Ukiangalia mambo yalivyokwenda yalikuwa ni makosa ya wazi” kuamini kuwa Cambridge Analytica ilifuta data, bila kufanya uchunguzi zaidi”
  • Hahisi “kama ” Facebook ina udhibiti
  • Kwamba wakati wote kutakuwa na kitengo kisicholipiwa cha Facebook, kunachoweza kulipiwa , kitengo ambacho hakina matangazo ya biashara cha mtandao wa kijamii”
  • “Kukabiliana na kauli za uchochezi wa chuki ” una kiwango cha juu cha makosa kuliko vile ninavyotaka “
  • Binafsi alihofia juu ya uwezekano wa upendeleo wa kisiasa kwenye kampuni yake

Kutokana na kuhojiwa kwa Bw Zuckerberg na seneti ya Marekani hisa za mtandao wa Facebook jana ziliongezeka hadi kufikia asilimia nne, nao wanasheria nchini Uingereza na Marekani wameanzisha mashtaka dhidi ya Facebook, Cambridge Analytica, na makampuni mengine mawili yanayounganishwa na kesi hiyo.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA