AndroidMaujanja

MUHIMU KUSOMA! Mambo 5 usiyopaswa kufanya kwenye simu yako ya Android

Tunatumia simu za mkononi kwa vitu vingi katika maisha yetu ya kitaaluma na ya kibinafsi. Kwa hiyo, tunapaswa kujaribu kuhakikisha zinadumu kwa muda mrefu kadri iwezekanavyo. Wengi huchukua tahadhari kama kuweka programu ya kupambana na virusi (anti-virus) na kufunga programu za nyuma, lakini hatua hizi ni muhimu sana? Hapa haya ni mambo matano unayofanya kwenye kifaa chako cha Android bila ya kujua kuwa yana athari.

simu-mkononi

1. Kutumia “task killers” au kufunga apps kwa njia ya manually

Wengi wetu hutumia “task killers” au kufunga programu moja kwa moja kupitia orodha ya hivi karibuni ya apps (recent apps menu). Lakini bila ya kutambua kwamba inaweza kuwa na madhara kwenye utendaji wa kifaa chako.

Tunapoanza kufungua app, sehemu ya data zake inakuwa imehifadhiwa kwenye RAM. Hii inamaanisha kwamba wakati wa kufungua app mara ya pili, itafunguka kwa haraka kwa sababu ya kuwepo kwa data zilizowekwa awali (cached data).

Ukiondoa programu/app kutoka kwenye orodha ya hivi karibuni ya apps (recent apps menu), au kufuta cache, data zilizohifadhiwa kwenye RAM zinapotea pia. Ikiwa unataka kufungua tena unapaswa kuanza mchakato huu tena.

Siku zote funga applications zako ikiwa ni lazima, kwa mfano, ikiwa zinatumia sehemu kubwa ya betri au inatumia rasilimali nyingi sana inapofanya kazi.

2. Kutumia programu zaidi ya moja ya antivirus

SOMA NA HII:  Jinsi ya Kurekebisha "Display Problems" kwenye Windows kwa kutumia Driver Update

Ikiwa unahitaji programu ya antivirus kwenye simu yako ya Android basi unapaswa kukumbuka kuwa inatumia sehemu kubwa ya RAM na betri: hizi ni programu kubwa zinafanya kazi kwenye simu yako muda wote. Lakini kuwa na zaidi ya moja haikufanya uwe salama. Ikiwa unaamua kutumia programu ya antivirus hakikisha unafanya uchaguzi sahihi kati ya programu nyingi zinazopatikana mtandaoni na tumia moja tu.

3. Kupuuza sasisho za programu (software updates)

Mfumo wa uendeshaji wa smartphone yako unahitaji kurekebishwa mara kwa mara ili kurekebisha upungufu kwa usalama. Mara tu unapoona sasisho, likubali. Unaweza hata kuweka simu yako ya Android ifanye sasisho moja kwa moja (automatically). Usalama wa simu yako itakushukuru. Itafanya kazi vizuri na kuwa na ufanisi zaidi.

4. Kupakua “applications” kutoka kwenye vyanzo visivyo vya uhakika.

Faili za APK za Android zinaweza kutumiwa ili kuwa na programu mbaya (malicious software) hivyo inaweza kuambukiza kifaa chako. Hakikisha downloads zako zote zinakuja kutoka kwenye vyanzo vya kuaminika kama Duka la Google Play.

5. Usianzishe “restart” tena smartphone yako

Kuna utata mwingi unaozunguka mada hii. Hata hivyo, kufanya rebooting ya kifaa chako mara moja kwa wiki ni ‘Afya’. Kwa upande mmoja, kumbukumbu zinahifadhiwa na data zilizohifadhiwa kwa muda mfupi (temporarily cached dat) zinafutika kwa sababu hazihitajiki tena. Kwa upande mwingine, wakati mwingine baadhi ya kumbukumbu huharibika na kufutika kwa data zilizohifadhiwa kwa muda, muda mwingine kunapelekea simu kuwa nzito.

SOMA NA HII:  Jinsi ya kuweka pesa kwenye akaunti yako ya Meridianbet na Kutoa kwa kutumia M-PESA

Je wewe unatumia njia gani kuhakikisha simu yako ya Android inadumu kwa muda mrefu ? Je unapendelea kufanya jambo gani kwenye simu yako? Tumia sehemu ya maoni kueleza ufahamu wako kuhusu simu za Android

Zinazohusiana

1 thought on “MUHIMU KUSOMA! Mambo 5 usiyopaswa kufanya kwenye simu yako ya Android”

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako