Elewa mambo 5 muhimu kuhusu betri ya simu na Kuchaji Simu


Tangu ulipoanza kutumia simu kuna mengi sana unaweza ukawa ushasikia kuhusu betri ya simu na njia nzuri za kuchaji simu yako. Pia utakuwa umeshaambiwa usifanye baadhi ya vitu ukiwa unachaji simu.

Leo tutakuelezea ukweli mambo muhimu kuhusu betri ya simu na kuchaji simu pia usalama wa betri za simu wakati tukiwa tunazichaji.

Kuna aina kuu mbili za mabetri yanatumika kwa sasa, kuna mabetri yanayotumia teknolojia ya Lithium-Ion (Li-ion) na Lithium-Ion-Polymer (Li-ion polymer/Lithium Polymer). Kuna teknolojia nyingi zilizokuwepo zamani ila kwa sasa hizi ndio zinazotumika zaidi.

Lithium-Ion (Li-ion) zinatumika zaidi katika simu wakati mabetri ya Lithium-Ion-Polymer yanatumika zaidi katika laptop na baadhi ya simu pia. Lithium-Ion-Polymer ndio teknolojia bora na salama zaidi na hii inaweza kuwa ni sababu kubwa zinatumika kwenye laptop nyingi.

  • Kutumia chaja ambazo si za makampuni ya simu zinaua simu

Hapana, hakuna ukweli kabisa katika hili ila ukweli ni kwamba usitumie chaja za ubora mbovu. Chaja feki si chaja zote ambazo hazitengenezwi na kampuni husika ya simu bali ni chaja ambazo zipo chini ya kiwango. Na hizi utazigundua kupitia bei zake, usikubali kumiliki simu ya gharama halafu ukawa mbahili katika kununua chaja za uhakika kisa bei zake. Cha muhimu ni kusoma kuhusu kiwango na ubora wa chaja inayofaa kwenye simu yako kabla ya kununua chaja isiyokuja na simu yako.

  • Usitumie simu yako wakati unaichaji

Si kweli, ni kweli zamani sana, kwa sasa teknolojia inayotumika kwenye chaja na simu ni salama kabisa. Cha kuhakikisha ni kwamba unatumia chaja zilizo na kiwango/ubora wa uhakika (original/quality). Kumbuka hapa haimaanishi ni kwamba lazima iwe ni yenye lebo/nembo ya kampuni husika bali hili ni suala la kuwa ni chaja yenye ubora wa uhakika.

  • Usizime simu yako kamwe!

Si kweli! Unashauliwa kuzima simu yako angalau hata mara moja kwa wiki kwa angalau lisaa. Simu kama vifaa vingine vyote vya umeme ni muhimu kupata muda wa kupumzishwa. Na jambo hili ndio linaboresha zaidi uhai wa simu yako.

  • Kuchaji simu usiku kucha kutaiua/haribu

Si kweli! labda kama unatumia simu iliyotengenezwa miaka ya 1980 :-). Teknolojia imekua sana, fahamu ya kwamba simu zote za siku hizi zitaacha kutumia umeme pale simu yako itakapochaji hadi asilimia 100! Itaacha kuchaji! Hakuna madhara! Ila hii haimaanisha ndio uiache kwa zaidi ya masaa 15! na pia kuhakikisha unaichaji sehemu inayopata hewa.

  • Subiri hadi chaji iwe chini kabisa au imeisha ndio uchaji

Hili sio kweli! Ukweli ni kwamba kuchaji mara kwa mara ndio kunasaidia zaidi kuongeza maisha ya betri yako. Kumbuka kuchaji mara kwa mara si kila baada ya dakika 5, bali ni kwamba usisubiri chaji iwe chini ndio uchaji, na si lazima ukiweka kwenye chaji usiitoe hadi imejaa.

Je makala hii imebadilisha uelewa wako kuhusu betri ya simu na Kuchaji Simu ? Tuambie kupitia sehemu ya maoni ni kitu gani ulikuwa unaamini kabla?

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA