Nyingine

MAMBO 10 AMBAYO KIJANA HUTAKIWI KUYAFANYA

Kuchagua Kazi.
Ni vigumu kupata Kazi ukiwa nje ya Kazi. Fanya Kazi uliyoipata upate Kazi unayoitaka.

Kuchagua sehemu ya kuishi /kufanyia Kazi.
Maisha ni safari ndefu, maisha ni popote, si lazima kukaa mjini. Hauwezi kujua ni sehemu gan iliyobeba mafanikio yako. Chagua sehemu yenye FURSA na si yenye MAGHOROFA.

 Kuishi bila kuwa na malengo.
Maisha si bahati mbaya au nzuri. Maisha ni mipango, Maisha yanaongozwa na malengo. Vile ulivyo leo ni matokeo ya jinsi ulivyopanga jana, na vile unavyoishi leo ndivyo kesho yako itakavyokuwa. PANGA KESHO YAKO SASA.

Maisha Ya kuiga.
Maisha yako si ya mwenzako, na ya maisha ya mwenzako si ya kwako. Si kila ukionacho ni lazima ufanye, chagua kipi cha kufanya na kipi cha kuacha. Kupitwa na jambo wakat mwingine sio USHAMBA bali ni BUSARA.

Kuishi juu ya kipato chako.
Ishi kulingana na vile ulivyonavyo na si usivyonavyo. Kuwa na Busara katika MATUMIZI uepukane na MADENI yasiyo na ULAZIMA. RIDHIKA NA VILE ULIVYONAVYO.

Kuishi bila AKIBA.
kuweka akiba ni TABIA sio kiwango kikubwa cha Pesa. Jenga tabia ya kujiwekea akiba. Haujui ni kipi kitakupata muda USIOTEGEMEA.

Kuishi kwa kutegemea MSHAHARA.
Mshahara haujawahi kutosha na hautatosha kama ukishindwa kuishi chini ya kipato chako na kuwa na njia mbadala za kuinua kipato chako. JARIBU NJIA ZINGINE MBALI NA MSHAHARA.

Kushindwa Kupangilia MATUMIZI ya Pesa.
Maamuzi yako ya pesa ndiyo yatakayoamua hali yako ya kiuchumi baadaye. Ni muhimu kujua kipi cha kununua, kwa wakati gani na kwa sababu gani. Jifunze kutofautisha kati ya dhima mfano: gari ya kutembelea na kitegauchumi mfano:nyumba au kiwanja. TUMIA PESA YAKO KUNUNUA KITEGAUCHUMI KULIKO DHIMA.

Kushindwa kutumia MUDA wako VIZURI.
Changamoto kubwa inayotukabili vijana ni kushindwa kujua namna ya kutumia vizuri muda. Tumia muda wako mwingi kujiendeleza ufahamu wako kwa kujisomea, kupanga malengo yako ya maisha, kujiuliza ni wapi ulikosea na nini ufanye ili urekebishe hayo makosa na muda mchache ufanye wa mapumziko na kufanya vitu vya kufurahisha akili yako kama kuangalia movie, mpira, kuingia kwenye mitandao ya kijamii Facebook, watsap n. k. Kumbuka muda ni rasilimali isiyoweza kurudishwa pindi unapopotea.

Kuoa bila ya kujipanga kimaisha.
Hii inawahusu wanaume, swala la kuoa ni pana sana na kila mtu ana vigezo vyake na mtazamo wake kufanikisha jambo hilo. Ila jambo la msingi ni hili, jiandae kwanza kiuchumi kabla hujaingiza majukumu mengine, unapooa ujue umekubali kusaidia upande wa mwanamke, upande wa familia yenu bila kusahau familia yako binafsi. Hata kama maisha ni kusaidiana na huyo utakayemuoa ila nafas yako kama mwanaume ITABAKI pale Pale.

Zinazohusiana

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Check Also

Close