Habari za Teknolojia

MallforAfrica Wameanzisha Tovuti Kwajili Ya Waafrika Kupata Moja kwa Moja Mamilioni Ya Bidhaa Kutoka eBay

Jukwaa la e-commerce barani Afrika “MallforAfrica (MFA)” imetangaza uzinduzi wa tovuti mpya kwa ajili ya wanunuzi wa eBay barani Afrika.

MallforAfrica ni e-commerce ambayo inawawezesha waafrika kununua mtandaoni kimataifa. Picha: MFA

 

Inapatikana katika nchi za Nigeria na Kenya, kabla haijaanza kupatikana katika nchi nyingine za Afrika, tovuti ebayforafrica.com inaonyesha kupanua uhusiano wake na eBay kwa faida ya wateja barani Afrika, sasa kuruhusu kupata mamilioni ya orodha kutoka eBay.com  moja kwa moja kwenye tovuti hiyo.

Akitangaza ushirikiano huo na kampuni kubwa ya biashara za mtandaoni kutoka nchini Marekani eBay, Mkurugenzi Mtendaji wa MallforAfrica Chris Folayan alionyesha furaha yake kuwa na uwezo wa kutoa huduma kwa wanunuzi wa bidhaa mtandaoni barani Afrika kwa kuwahakikishia upatikanaji wa mamilioni ya bidhaa.

“We are thrilled to expand our relationship with eBay,” amesema Folayan, kwa mujibu wa taarifa ya eBay.

“Mpaka sasa, wamekuwa washirika wakubwa na tunatarajia kuendeleza ushirikiano wetu. Jambo la muhimu zaidi, tunategemea kuwa na uwezo wa kutoa mamilioni ya bidhaa kwa wateja ambao wanafanya manunuzi mtandani, “aliongeza.

Ilianzishwa mwaka 2011, MallforAfrica inawezesha waafrika kununua bidhaa kwa wauzaji wa mtandaoni zaidi ya 200 kutoka Marekani na Uingereza kwa njia ya e-commerce ya jukwaa/platform yao, wakiendelea kuzingatia kauli mbiu yao, “shop global, pickup local”.

MallforAfrica na eBay walianza ushirikiano wao mwaka 2016 kwa uzinduzi wa app ya eBay ‘Powered by Mall For Africa’ katika nchi za Nigeria, Kenya, Ghana, na Afrika Kusini, kwa mujibu wa Tech Crunch.

Tovuti mpya itawafikia wateja wa Afrika kwa bei zenye uwazi ambayo ni pamoja na bei ya bidhaa, kusafirisha kimataifa, utunzaji, ushuru na ada, inaruhusu mnunuzi kuelewa kiasi cha mwisho cha manunuzi yake mtandaoni kitakavyokuwa.

Wateja pia watakuwa na uwezo wa kufuatilia hali ya “packages” zao kutoka mwanzo hadi mwisho, na ebayforafrica.com itatoa faida sawa na wanazofurahia wanunuzi wa Marekani  katika suala la “eBay returns & exchanges program”.

SOMA NA HII:  Ifahamu treni yenye spidi kali zaidi duniani

Mada zinazohusiana

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako