Sambaza:

Mkutano wa nchi zenye uchumi mkubwa G7 ulifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita ,ukiwa umelenga kupunguza shughuli zinazoongeza uzalishaji wa hewa chafu ili kupuguza athari za mabadiliko ya tabia nchi kama ilivyokubaliana na nchi takribani mia mbili.

Makubaliano ya mabadiliko ya tabia nchi,Paris

Lakini, rais wa Marekani,Trump hajaliridhia swala hili na tayari vyombo vya habari vya marekani vinasema rais Trump anatarajia kutangaza kujitoa kwenye makubaliano ya mabadiliko ya tabia nchi yaliyowekwa mjini Paris, Ufaransa.

Rais Trump mwenyewe aliandika katika ukurasa wake wa Twitter kuwa anatoa tangazo hilo hivi karibuni.

Kujitoa katika harakati hizo za mabadiliko ya tabia nchi ni miongoni mwa vipaumbele ambavyo alivitaja wakati wa kampeni zake za urais ingawa hivi karibuni rais huyo alikaririwa kusema kuwa bado hajafanya maamuzi.

SOMA NA HII:  TBL Kujenga Kiwanda Kikubwa cha bia mkoani Dodoma

Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako