Makosa 6 ya kifedha yanayofanywa na wamiliki wa biashara mpya na jinsi ya kuyaepuka


Wajasiriamali huwa wanangalia fursa kila mahali kutanua mipaka na kugundua mambo mapya kuhusu wao wenyewe na sekta ambazo wamewekeza nguvu zao. Hata hivyo, nia hiyo muda mwingine huleta uwezekano mkubwa wa kufanya makosa.

Hapa chini kuna makosa makubwa ya kifedha ambayo wamiliki wa biashara huyafanya, na jinsi ya kuyaepuka.

1. Kutokuwa na akaunti tofauti za biashara na binafsi

Hakuna njia ya mkato kwenye suala hili. Hata kama unajishughulisha wewe mwenyewe kama freelancer, huwezi kuweka fedha zako tofauti ? jifunze kuweka akiba zako sehemu tofauti, ni muhimu kuwa na akaunti tofauti kwajili ya biashara na mambo binafsi.

Kufanya jambo hili mwanzoni kabisa itafanya iwe rahisi kufanya uhasibu wa biashara yako, kupanga mpango wa kodi na bajeti kwa miezi kadhaa inayokuja.

2. Mara moja kufanya manunuzi makubwa kwa ajili ya biashara

Kama mmiliki mpya wa biashara, inaeleweka kutaka laptops bora zaidi, tovuti ya kisasa, ofisi yenye ufanisi, programu bora zaidi na wafanyakazi wenye vipaji vikubwa ili kusaidia kukua kwa kampuni.

SOMA NA HII:  TCRA imezindua mfumo wa usajili laini kwa kutumia alama za vidole

Hata hivyo, ikiwa unataka kufanya manunuzi makubwa mwanzoni mwa biashara yako, fikiria maamuzi hayo kwa makini sana. Baadhi ya gharama kama kutengeneza tovuti au kuhudhuria mkutano wa tasnia ya biashara itakuwa lazima kulingana na aina ya biashara unayoanzisha. Lakini unatakiwa kuwa na uhakika kuwa gharama zitarudisha mapato kwa muda mfupi.

3. Kufanya manunuzi makubwa ya kibinafsi

Hata kama umetenganisha akaunti zako za kibinafsi na za biashara, mara nyingi matukio yanajitokeza ambayo yanapelekea kutumia fedha zako za kibinafsi ili kuwezesha mahitaji ya biashara, kama vile upanuzi kwenye soko jipya au kampeni ya masoko ili kuongeza faida ya kampuni.

Ikiwa umekimbilia kununua gari, nyumba au gharama nyingine kubwa za kibinafsi na kuna kitu kimetokea kwenye biashara yako na haukukitarajia, kinasababisha ushindwe kujilipa mwenyewe mwezi ujao, utaangushwa na kiasi kikubwa cha gharama za kibinafsi. Kuwa kama konda kadri iwezekanavyo katika biashara yako na maisha yako binafsi wakati unapokuza kampuni yako mpya.

SOMA NA HII:  Mbinu 6 Zinazoweza Kukuza Kazi za Mjasiriamali

4. Kutokuweka bajeti ya nzuri kwajili ya biashara yako

Unaweza kuendesha biashara yako bila mpango mzuri wa siku zijazo, lakini utakuwa na wakati mgumu sana kufanikiwa bila angalau, kuwa na bajeti ili kusaidia kuongoza kile unachoweza na usichoweza kumudu kutumia kila mwezi.

Kama mmiliki na mwanzilishi wa biashara, kazi yako ni kuiongoza biashara yako mpya kuleta faida, na unaweza kufanya hivyo ikiwa una bajeti iliyopangwa kwa umakini kwa ajili ya uendeshaji, kujitangaza na gharama nyingine. Kuwa na bajeti ya wazi huongeza nidhamu ya kifedha na hufafanua ramani kwaajili ya ukuaji wa biashara.

5. Kutokuweka akiba kwajili ya nyakati ngumu na dharura

Unatakiwa kujiwekea mfumo wa kuweka akiba kwajili ya gharama zisizotarajiwa. Unaweza kuita mwokozi wa siku zijazo, kwa  sababu kutakuwa na wakati ambapo kuna vitu vimetokea na unatakiwa kufidia gharama haraka.

SOMA NA HII:  Mbinu ya kuongeza uaminifu kwa wateja kwa kutumia Email za kibiashara

Ili kujiandaa kwajili ya wakati huo, ni busara kuweka angalau fedha ya miezi mitatu katika mfuko wa dharura kwa ajili ya gharama zako zote za biashara na binafsi.

6. Kutokuwa na ujuzi wa maswala ya fedha

Ni rahisi sana kupoteza pesa kuliko kuzipata. Wakati uamuzi mdogo wa kifedha unaweza kusababisha biashara yako kufa, kushindwa mara nyingi zaidi kuliko kutokufuata mfululizo wa maamuzi mabaya na makosa ya kifedha. Unaweza kuepuka makosa haya kwa kutoa kipaumbele zaidi kwenye maelezo ya mtiririko wako wa fedha binafsi na biashara kila mwaka.

Panga bajeti yako, kufuatilia matumizi yako, weka akiba, weka mstari kati ya biashara na maisha binafsi, na siku zote ufikirie gharama zako na jinsi zinavyoweza kuzalisha mapato ya baadaye kwajili ya kampuni.

Toa maoni yako!

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *