Habari za TeknolojiaNyingine

Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu kuhusu msiba wa watu 32

Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu

Makamu wa Rais Mama Samia Hassan Suluhu amesema wanafunzi wa shule Lucky Vicent waliofariki kwa ajili juzi ni malaika ambao hawana hatia. Akizungumza katika uwanja wa Sheik Amri Abeid, Arusha muda mfupi uliopita, Mama Samia amesema ajali na msiba ulitokea ni wa aina ya pekee kwa kuwa umegusa nyoyo za watanzania wote.

‘Wamendoka kwa matendo yasiyo ya kwao, ni watoto waliokuwa wanaenda kujifunza lakini Mungu amewachukua katikati, msiba huu kwa kweli umetupa majonzi mengi na wakati ni huu mgumu, hatuna la kusema ila tuwaombe Mungu awapokee salama,” alisema.

Pia alichukua nafasi hiyo kuitaka serikali na jamii kwa ujumla kutufumbua macho katika kufanya marekebisho ya mambo mengi ambayo yanakosoro na kuleta maafa kama haya.

“Naomba nichukue nafasi hii kupaza sauti yangu kuwaomba sana ndugu zangu madereva kuwa waadilifu na kuwa makini wanapokuwa barabarani, serikali yetu inapiga vita utumiaji wa vilevi wakati unapoendesha, tunapiga vita utumiaji wa dawa za kulevya kwa sababu tunajua ni moja ya sababu inayoleta hasara ya namna hii.

 

“Madereva wanapochukua abiria wahakikishe magari yanachukua abiria kwa uwezo yalitengenezewa, watanzania hatuhimili na haipendezi kila siku kusikia kuna ajali na kupata misiba,” alisema.

Aliongeza kuwa waombolezaji katika kipindi hiki hawapo pekee yao bali taifa lipo pamoja nao na watanzania wote wanasimama kwa maombi na sala.

“Huzuni hii si yenu, bali ya ni ya taifa na Afrika Mashariki kwa ujumla, kwa kuwa kazi ya Mungu haina makosa tunaamini aliwapenda sana watoto wetu,” alisema na kuongeza.

 

“Nitoe wito kwa Wizara ya elimu, jeshi la polisi, wazazi na walezi kuwa makini kuhakisha sheria za usalama barabarani zinazingatiwa kwa kuchukua hatua za kulinda watoto wetu na watanzania kwa ujumla wao ,” alisema.

Zinazohusiana

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *