Sambaza:

Producer mkongwe P Funk amemjibu Master Jay baada ya kusema msanii wake hana kipaji, Majani amesema Master Jay hatakiwi aongee kwa kuwa alikuwa akimletea wasanii wabovu na P funk kuwapotezea akitolea mfano wa msanii Ndugu Sulukuchu na John walker ambaye alikuwa mburudishaji kwa style yake ya ulevi na sio kuimba, Majani amesema:

“Unajua nilipoanza kumtoa Juma Nature waliniambia siyo msanii ila ni MC cartoon na kwamba hawezi kuwa kama Solo au Prof Jay kwa hiyo nilichekwa sana Nature pia alisemwa sana lakini nachomshukuru Mungu amenipa uwezo wa kumtambua mtu mwenye kipaji na najua huyu ata’hit au la! na kwa Harmorapa nina imani atafika mbali sana kwa hiyo J yeye asizungumze anyamaze tuu,”.

Pia, Majani amemuuelezea Harmorapa kama kijana anayestahili kuwapo kwenye sanaa hata kama si mwanamuziki lakini ni mburudishaji ambaye ana kipaji cha kuwafanya watu wafurahi hivyo hatakiwi kuwa nje ya sanaa:

“Harmorapa siyo msanii direct, kuna rapa, MC na Entertainer sasa dogo ni Entertainer. Master J kama anakumbuka kuna kipindi alimleta yule Sulukuchu studio anaimba ndugu Sulukuchu, sasa yule msanii gani lakini kuna John Walker (RIP) yule alikuwa mburudishaji kwa style yake ya ulevi kwahiyo Harmorapa anaingia kwa mtu kama Walker, watu wakipenda anachofanya ndiyo burudani yenyewe,” alisema.

Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako