Maujanja

Majibu 9 ya maswali unayojiuliza kuhusu Teknolojia ya sasa

Kila siku unavyotumia vifaa vya teknolojia matatizo mbalimbali hujitokeza na kukuacha na maswali mengi kichwani, miongoni mwa maswali hayo ni kama Nitafanyaje endapo kompyuta yangu imeingiliwa na wezi wa mitandao?, Nitafanyaje kulinda betri langu kwa muda mrefu?, Ni virus gani ambao ni wabaya kwenye kifaa changu?, Kuna ubaya gani kama nitatumia Public WiFi networks? Na mengine mengi.

Leo tumewasogezea baadhi ya maswali ambayo huwa tunaulizwa na wadau mara kwa mara na majibu yake, Soma hapo ili ujifunze zaidi huenda pia hata wewe kuna baadhi ya maswali yalikuwa yanakusumbua.

1. Nitafanyaje kulinda betri langu la laptop au Simu kwa muda mrefu?

Kuna baadhi ya watu huwa wanasema kwamba Ni lazima kumaliza chaji yote kwenye betri lako kabla ya kuchajisha, au kwamba unapaswa kutunza kati ya 40% na 80% wakati wote. Sheria hizo tayari zimekwisha muda wake kwa sasa hauna mambo hayo kwa kuwa vifaa vingi kwa sasa vinatumia Lithium Ion batteries, ambayo huwa inakuwa makini kwa mambo hayo. Ukweli ni kwamba baada ya betri yako kufikia 100% basi chomoa au disconnect kwenye umeme na uitumie kifaa chako, kiukweli maisha ya betri kwa sasa linalindwa sana, na tambua kwamba hakuna kitu kisichokuwa na mwisho hata betri lako wakati wowote linaweza kufa kwa sababu zingine na si kwa sababu kama niliyoelezea mwanzo kama watu wanavyoongea. Kinachotakiwa ni kuzingatia juhudi yako ya kupata maisha bora ya betri yako ya iPhone, Android phone, hata laptop.

2. Je, Viruses, Trojans na Malware wengine huwa kwa kawaida wanafanya nini?

Kila mtu anajua kwamba viruses na trojens ni wabaya, lakini watu wengi hawajui jinsi gani hasa wanafanya kazi. Virus ni program ambazo zinajicopy zenyewe na kuathiri kompyuta, zinasambaa kutoka sehemu moja hadi nyingine. Trojans, kwa upande mwingine, ni application ambazozinaonekana kawaida, lakini kwa siri zina codes ambazo zinafanya kitu kingine- kama kudhibiti kompyuta yako. Tunapendekeza usome maelezo zaidi juu ya Viruses na Troans kwa undani zaidi. Na hakikisha unatumia Antivirus nzuri ili kudhibiti Virus kwenye kifaa chako.

SOMA NA HII:  Orodha ya Maneno ya Teknolojia na Tafsiri zake kwa Kiswahili

3. Kuna ubaya gani kama nitatumia Public WiFi netwaorks?

Habari yeyote unayoituma au kupokea kupitia public WiFi huwa inapatikana kwa mtu yeyote mwenye upeo wa kutafuta habari hiyo. Mfumo huo wa connection unatoa ruhusa kwa wezi wa mitandao yaani hackers kupekua habari zako kiurahisi, Sasa unapaswa kutumia WiFi network ambayo inalindwa na password nah ii itakusaidi wewe kulinda taarifa zako. (Mfano wa Public WiFi Network, Kwa Dar es salaam inapatikana Stendi kuu ya dala dala Ubungo,Mlimani City na sehemu zingine)

4. Hivi ni kweli natakiwa kubonyeza eject USB Flash kabla sijaichomoa kwenye kompyuta?

Cha ajabu ni kwamba hivi kwa nini kompyuta yako huwa inakuonya kuhusu ku eject USB driver zote kabla ya kuondoa? Ni kwa sababu ya kompyuta kutumia kitu kinachoitwa Write Caching ili kuboresha utendaji: kama una copy kitu kwenye Drive yako, itakuambia imemaliza kazi, lakini ni kweli husubiri mpaka kazi nyingine ya kufanya hivyo inaweza kufanya zote kwa mara moja. Ufanisi, sawa? Unapo bonyeza eject, PC yako inamaliza vitu vyote katika foleni ili kuhakikisha hakuna data yeyote inayopotea. Windows inafanya kazi bora ya kuepuka matatizo ya OS X na Linux, lakini tunakupendekeza uanze kubonyeza eject kabla hujaondoa drive yako.

5. Kitatokea nini endapo Site ninayoitumia imevamiwa na hackers?

Kama una akaunti kwenye hiyo site, na akounti yako uliyoweka ni weak password basi nawe pia unaweza kuathirika pia, lakini kama paasword yako ni strong password hutoweza kuathirika na lolote kwa muda huo, kinachotakiwa kufanya ni kuingia kwenye hiyo site na umepata Access basi jaribu kuingia kwenye Akaunti yako na ukiona ipo sawa unaweza kufanya backup ya data zako zote, na kusubiri mpaka pale site itakapokuwa vizuri na baada ya kupata taarifa kuwa wame upgrade na kuthibiti hackers.

SOMA NA HII:  Goal Technology kuanza kutumika kwa mara ya kwanza Afrika

6. Kwanini natakiwa kufanya Resetting ya Router yangu?

Ni hadithi ya zamani kidogo: Internet huwa inapatwa na finicky, hivyo unplug router yako, kisha plug tena na ghafla magically kufanya kazi tena. Lakini kwanini hii itokee, kweli? Inaweza kuwa idadi ya mambo: Huenda ni Overheating, labda hudhoofishwa kutoka msongamano mkubwa (kama BitTorrent), au labda ni crappy ya router tu. Bahati nzuri, kuna mambo mengi unaweza kurekebisha. Hakikisha unapo unplug unasubiri baada ya sekunde kama 10 kabla ya kurudishia.

7. Ni kweli nahitaji kulinda kuhusu My Privacy Online?

Kila mtu anajua ni mbaya ikiwa mtu fulani ataiba nywila au kadi yako ya mkopo, lakini watu wengi wana apathetic nyingi kuweka kwenye Facebook, blog yao binafsi, au mahali popote pengine. Data zako binafsi zinastahili kulindwa, ingawa, kama unafikiri hivyo au la. Si tu kuwa takwimu zinazo tolewa na makampuni na serikali ndio zina nguvu zaidi kufuatilia, lakini inaweza kufanya kuwa rahisi kwa mtu kwa kuiba utambulisho wako, hata kama ni haionekani kama hiyo. Plus, huwezi kujua ambapo kwamba data wanaweza kuishia siku moja, na nani anaweza kuiona (waajiri watarajiwa, kwa mfano).

8. Je, tunahitaji Antivirus kwenye simu zetu za smartphone?

Kama simu yako unapoinunua dukani hukupakua App yeyote kutoka Play Store kwa mfano Facebook, Whatsapp, Instagram na zinginezo basi wala huitaji kutumia antivirus, lakini tambua kuwa unaweza usifanye hivyo lakini unarushiwa nyimbo kutoka simu nyingine, je? unahakika simu yake ipo safe? Hivyo basi kwa ulinzi sahihi wa simu yako kwa kuwa unaweza kupakuwa App mbalimbali na Kurushiwa vitu mbalimbali kutoka kwa rafiki yako ni muhimu kuwa na Antivirus kwanye simu yako.

9. Nifanye nini kama Simu yangu inafunguka taratibu/ run slow?

i.Toa Program zote ambazo hazina maana kwako ama huzitumii. Program (kwa jina maarufu SOFTWARES) ni MAAGIZO maalum ambayo husaidia jambo flani kufanyika. Mfano unapopiga simu, program/software inayohusika (inaitwa Phone) hukuwezesha wewe (User) kwa kutumia vitu vinavyoshikika kama vile Speker na Microphone ya simu yako (Hardware) kufanya mawasiliano. Sasa kama kuna program nyingi kwenye mfumo wa simu yako ambazo pengine hazina faida kwako zitaleta tu UZITO. Nenda Settings>Apps kisa UNISTALL program zote ambazo hazikustahili. Kwa wale wenye “Root access” wanaweza hata ku uninstall SYSTEM APPS. Dowwnload program iitwayo ‘Uninstall’ yenye icon nyekundu Playstore itakusaidia. Kua makini usijetoa program za muhimu.

SOMA NA HII:  #MHKutokaMaktaba!! Tujikumbushe Watangazaji wa Zamani wa Redio na TV

ii. Epuka kutumia program nyingi zinazofanya kazi moja. Kuna Apps/Program, sio kwenye simu tu, hata Kompyuta, ambazo lengo lake ni moja. Mfano kuna simu ukiitumia kufungulia ‘pdf document’ inakuuliza Complete the action using 1. Adobe Acrobat, 2. Drive PDF Viewer, 3. WPS Office, 4. PDF Reader, na hata Zaidi. Sasa hapo mtumiaji unapaswa kuchagua angalao mbili ukushindwa sana na nyingine zitoe zote. Huo ni mf tu, kuna App nyingi ambazo kazi yake ni moja na inawezekana zipo kwenye System yako.

iii. Tumia Antivirus MOJA inayoaminika. Kuna antivirus moja niliijua kupitia hili kundi letu, inaitwa CM Security. Nilipoi download playstore ilinishawishi kutoa iliokuwepo; na kila nilipojaribu nyingine nilijikuta nairudia tu. Hii ina ‘FREE FEATURES’ nyingi sana!! Sivyo nilijikuta natoa program nyingine nyingi!! Niliona kipengele flani ndani kiitwacho ‘Clean up junk’ nikatoa CCleaner, nikaona ‘Phone Boost’ nikatoa DU Booster, nikaona Call blocking nikatoa Call blocker root, nikaona ‘Power boost’ nikatoa DU Battery Saver…… Sasa kama umenielewa itakusaidia sana!! Kuna kipindi nilijikuta nimeweka program nyiiiiiingi, sijui hii ni ya kutunza chaji, sijui hii ni yak u boost simu, sijui hii ni yak u OPTIMIZE….lakini mwishoni nikagundua ni za kibiashara tu, na zilikua zinaongeza uzito Zaidi na zaidi kwani nazo zina operate chini kwa chini (background) na hata kufanya simu iwe ya moto.

Mada zinazohusiana

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako