Maelezo Kuhusu Matoleo Ya Microsoft Windows 8/8.1


Unachotakiwa kufahamu kuhusu matoleo mbalimbali ya Windows 8 / 8.1.

Windows 8 imetolewa kwa umma mwishoni mwa mwaka 2012, lakini wengi wenu huenda bado mnatumia programu ya mfumo wa uendeshaji wa zamani. Katika kila toleo  la Windows kuna matoleo mbalimbali ya OS hutolewa pia. Kwa kweli, ipo mpya tangu Windows 8 ilipokuwa ya kwanza – na pengine ya mwisho – toleo la PC la mfumo wa uendeshaji wa Microsoft linalojumuisha ARM processors.

Maelezo Kuhusu Matoleo Ya Microsoft Windows 8/8.1-mediahuru

Hakuna shaka kuhusu hilo, kuna mabadiliko makubwa katika Windows 8 / 8.1 ikilinganishwa na Windows 7 na matoleo mengine ya awali ya mfumo wa uendeshaji wa Windows. Hapa tunaangalia matoleo yote katika lugha rahisi ya kiswahili.

Matoleo ya Windows 8.1 / 8.1

Kama mtumiaji wa Windows wa awali utatambua kwamba matoleo mapya yana maana kubwa kwa kurahisisha upatikanaji wa bidhaa. Fikiria Windows 7 peke yake ilikuwa na matoleo sita tofauti: Starter, Home Basic, Home Premium, Professional, Ultimate na Enterprise. Woo! Ni orodha ndefu. Windows 8 / 8.1 imeunganisha matoleo hayo kuwa matatu tu, pamoja na kuongeza toleo jipya la ARM processors.

SOMA NA HII:  Jinsi ya kubadili mpangilio wa keyboard ya kompyuta kuwa Dvorak keyboard

Windows 8/8.1 (For the Consumer)

Plain old Windows 8 / 8.1 ni toleo la watumiaji wa kawaida wa OS hiyo. Haijumuishi vipengele vingi vya biashara kama vile drive encryption, group policy na virtualization. Hata hivyo, utakuwa na uwezo wa kutumia Windows Store, Live Tiles, Remote Desktop Client, VPN Client na vipengele vingine.

 Windows 8/8.1 Pro (For Enthusiasts,  Professionals & Businesses)

Pro ni toleo la Windows 8 kwajili ya PC enthusiast, na business/technical professionals.

Inajumuisha kila kitu kilichopatikana katika 8 plus na vipengele kama BitLocker encryption, PC virtualization, domain connectivity na PC management. Ni kitu uchotarajia kutoka kwa Windows kama ni mtumishi mkubwa au unafanya kazi katika mazingira ya biashara.

Toleo hili linajumuisha kila kitu ambacho kimo kwenye Windows 8 Pro, lakini ina lengo la wateja wa biashara na mikataba ya Assurance Software.

Windows 8/8.1 Enterprise (For Large Scale Corporate Deployments)

Toleo hili linajumuisha kila kitu ambacho kimo kwenye Windows 8 Pro, lakini ni maalumu kwa enterprise customers na Software Assurance agreements.

SOMA NA HII:  Fahamu Faida & Hasara za Kutumia Kompyuta ya Windows 8

Windows 8 / 8.1 RT (ARM au WOA)

Windows 8 / 8.1 RT (Windows Runtime AKA WinRT) ni toleo jipya zaidi kwenye orodha ya matoleo ya Windows. Imeundwa maalumu kwa ajili ya vifaa vya msingi vya ARM kama tablets na PC zenye uwezo wa ARM.

Mfumo wa uendeshaji utawekwa kabla kama vile tablet inavyoendeshwa na Android au iOS huku mfumo wake wa uendeshaji ukiwa umewekwa (preinstalled) na upo-configured . Hii ina maana kwamba huwezi kupakia RT kwenye tablet yoyote au kifaa kingine ulicho chagua.

Jambo zuri kuhusu Windows RT ni kwamba hutoa encryption ya kifaa na “touch-enhanced Office suite” kama sehemu ya mfumo wa uendeshaji (operating system), hivyo hakuna haja ya kwenda kununua nakala ya “Office” au wasiwasi juu ya kuibiwa kwa data zako.

Kumbuka: ARM ni processor architecture inayotumiwa katika vifaa kama simu za mkononi, tablets na baadhi ya kompyuta. WOA inahusu Windows ya ARM au Windows 8 RT ambayo inaendesha vifaa vya msingi vya ARM (ARM-based devices).

SOMA NA HII:  Format memory card, flash drive (Njia ya kuondoa virus kabisa)

Tatizo ni kwamba Windows RT toleo lake  la desktop linafanya kazi na Office suite na Internet Explorer tu.

Naweza Kuupgrade hadi Windows 8?

Windows 8 / 8.1 inaweza kuwekwa kama maboresha kutoka Windows 7 Starter, Home Basic na Home Premium. Watumiaji wanaotaka kuupgrade hadi 8 Pro watakiwa kuwa na Windows 7 Professional au Windows 7 Ultimate.

Ikiwa unatumia Windows Vista au XP, hapa unatakiwa kuwa na PC mpya . Ikiwa PC yako ina vifaa sahihi, unatakiwa kununua toleo kamili la Windows 8 ili kuboresha. Microsoft tayari imehamia kwenye Windows 10, ambayo pengine ni chaguo bora kuliko Windows 8.1. Hasa kwa vile unaweza kufanya maboresha kutoka Windows 7 hadi Windows 10 bure kabisa mpaka mwishoni mwa Juni 2016.

Ikiwa unasisitiza kuhamia kwenye Windows 8.1, hata hivyo, unaweza kununua nakala yako mtandaoni kwa karibu $ 100.

Ikiwa unataka kujifunza zaidi kuhusu utofauti wa matoleo haya, hakikisha kunaingia kwenye Blogu ya Microsoft inayoelezea tofauti zote na vipengele kati ya matoleo haya.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA