Madeni !! Ofisi za TFF za fungwa na TRA

Comment

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imezifungia ofisi za shirikisho la soka Tanzania (TFF).

TRA kupitia Kampuni ya udalali ya Yono Auction Mart imewataka wafanyazi kuacha kila kitu cha shirikisho hilo ndani.

Mkurugenzi wa huduma na elimu kwa mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo amethibitisha hilo na kusema TFF haikutimiza walichokubaliana kuhusiana na wanachowadai. alipo ongea na chombo kimoja cha habari

“Ni kweli tumezifunga na hiyo ni hatua ya mwisho kwetu kufanya hivyo. Tulikubaliana kulipa tunachowadai na muda umepita,” alisema.

Alipouliuzwa kuhusiana na kiasi: “Haya ni masuala ya sisi na wenyewe.”

Yono ndio waliohusika katika kuzifunga ofisi hizo na kuwataka wafanyakazi wote kutotoka nje ya ofisi na kuacha kilakitu ndani.

Up Next

Related Posts

Discussion about this post