Nyingine

MABASI YA ABOOD NA HAPPY NATION YAPATA AJALI MLIMA KITONGA YALIKUWA YAKITOKEA MBEYA KUELEKEA DAR

Mabashi ya abiria Abood na Happy Nation kutoka Mbeya kwenda jijini Dar es salaam yamepata ajali mlima Kitonga leo mchana.

Taarifa rasmi kutoka kwa Mkuu wa Kikosi cha Zimamoto Mkoa wa Iringa Kamanda wa Jeshi la zimamoto mkoa wa Iringa Kenedy Komba akiwa eneo la tukio ametihibitisha kutokea kwa ajali hiyo, akielezea kuwa taarifa za awali majeruhi ni 12 na kati ya hao majeruhi watatu wamekimbizwa hospitali ya Rufaa mkoa wa Iringa kwa matibabu zaidi, na kwamba hakuna vifo vilivyotokea katika ajali hiyo.

Mmoja wa Mashuhuda wa tukio hilo alieleza kuwa ajali hiyo imetokea baada ya basi la Abood kukosa breki na kuligonga roli la FM ambalo halikuanguka ila liligonga Fuso iliyokuwa imebeba ndizi na kutumbukia korongoni baadae likaigonga basi la Happy Nation na mabasi yote kutumbukia korongoni .

Soma na hizi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Close