Home Nyingine Mabadiliko ya muziki wetu wapi tunakwenda ?

Mabadiliko ya muziki wetu wapi tunakwenda ?

0
0


Muziki unaundwa na radha, ujumbe ufuata kutegemea mazingira na aina ya muziki, Wasanii kama Prof jay walifanya kazi ya ziada kuwashawishi na kuvuta mashabiki ili wapende muziki wa rap haikutosha tu ujumbe bali ni pamoja radha.

Lakini nikisikiliza bongofleva za sasa Kichwa kinaniuma kwa sababu najiuliza wasanii wa sasa ni wapi wanaupeleka muziki huu maana kila kukicha wasanii wa bongo fleva wanaongezeka lakini hakuna cha maana wanachoimba zaidi ya kucopy nyimbo na matusi.

Zamani muziki ulikua muziki wasanii waliimba vitu vingi ambavyo vinaendana na maisha yetu halisi. Jiulize  ni kitu gani ambacho Prof J , Mr 2 na Afande sele hawajagusa ? Usisahau Jay mo na wenzake hakuna walichoacha hakuna wasichokigusa.

Ila kwasasa mambo ni tofauti nashindwa kujua nchi yetu wasanii wake wanaimba nini watu wote wanataka kuimba kama Wanaigeria, Afrika ya kusini ama Wamarekani , asilimia kubwa ya nyimbo zinazotoka hivi sasa zina radha za nchi nyingine kabisa na hazina chochote kinachoendana na muziki asili wa Tanzania ama maisha halisi ya Mtanzania wapi tunaenda wapi tumekosea ?

Je ni kweli wote tunapenda Wanaigeria wanavyoimba jibu rahisi ni hapana ni baadhi tu. Je kwanini tunawaiga ?

Mimi naona ni utumwa wa kifikra kwamba wanachofanya wao ni kizuri kuliko chetu kitu ambacho ni uongo pia media zetu kusupport sana wasanii wa nje kuliko ndani na kuamini ukifanya aina flani ya muziki ndo utateka soko…..

Wakati umepita na mambo yake na muziki wake ila zimekuja hela zimebadili muziki wetu hatuna radha ya muziki wetu nikisikia kwaito nitajua hii kwa madiba nikisikia mdundo huu najua hawa wanaigeria Ila Vipi hapa kwetu nyimbo kama “Mugacherere, KOKORO na nk ni radha za wapi?

(0)

LEAVE YOUR COMMENT

Your email address will not be published. Required fields are marked *