Nini maana ya over 2.5 na under 2.5 kwenye kubeti mpira


over 2.5

Inaweza kuwa kitu cha kawaida kwa wazee wa kubeti mpira mara kwa mara au wafanyabiashara ya kubeti, lakini kwa mtu anayependa kutabiri mpira wa miguu mara moja moja, anayeanza kubeti, au shabiki wa soka anayetaka tu kujua option za mpira wa miguu kwenye kubeti, anaweza asielewe nini maana ya over 2.5 na under 2.5 kwenye magoli ya mechi za mpira wa miguu.

Ni wazi huwezi kuwa na goli nusu (0.5) katika mechi, hivyo haishangazi kuwa inachanganya kidogo kwa wale wasiojua maneno ya kutabiri mpira.

Kwa hivyo kuweka vitu sawa, haya ndio majibu ya maswali mawili yanayoulizwa mara kwa mara ….

Je, nini maana ya Under 2.5 ?  Ukichagua Under 2.5 hii ina maana kwamba katika hiyo mechi magoli yatakayofungwa yasizidi mawili, yaani iwe ni kuanzia 0 na yasizidi mawili. Hii haijalishi nani kamfunga mwenzake ili mradi tu jumla ya magoli yasizidi mawili hata kama wakifungana 0-0, 1-0, 0-1, 2-0, 0-2 au 1-1 ni sawa.

Je, nini maana ya Over 2.5 ? Ukichagua Over 2.5 ina maana hiyo mechi iwe na magoli zaidi ya mawili, yaani kuanzia 3 na kuendelea na pia haijalishi nani kafunga au wamefunganaje. Hii inaweza kuwa na namba yoyote ya mabao, 2-1, 3-0, 6-0, vyovyote vile, ili mradi jumla ya magori ni 3 au zaidi.

Over/Under 2.5 ni kwa dakika 90 za mchezo (pamoja na dakika za nyongeza) kwenye kubeti. Hii inamaanisha muda wa ziada katika mechi za kikombe, nk, hazijumuishwi.

Pia ni moja ya option maarufu zaidi ya kubeti kwenye mpira wa miguu. Sehemu ya sababu ya kuwa hivi ni kwa sababu odds huwa zinashawishi zaidi, ni moja ya mkeka ambao kuna 50/50 kati ya wewe na muhindi.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA