Nyingine

Maamuzi ya mahakama kuu kuhusu ombi la Mbowe kutaka asikamatwe na Polisi

Mahakama Kuu ya Tanzania leo March 2, 2017,imetupilia mbali maombi yaliyowasilishwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe ya kutaka asikamatwe hadi kesi yake ya kikatiba dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda itakapomalizika.

Mwanasheria nguli Tanzania Generali Ulimwengu akiwa mahakamani kama wakili wa Freeman Mbowe

Jopo la majaji wakiongozwa na Jaji Sekieti Kihiyo wameutaka upande wa mleta ombi hilo kufanyia marekebisho ya kifungu kwenye maombi ya Freeman Mbowe kuzuia kukamatwa na Jeshi la Polisi na kumuweka ndani wakati kesi ya msingi ikiendelea

Uamuzi huo wa majaji umefikiwa kutokana na pingamizi la jamhuri lililowasilishwa na Wakili wa Serikali Mkuu Gabriel Malata kuiomba kuyatupilia mbali maombi hayo kwani hayana msingi kisheria.

Katika hatua nyingine, mwanahabari nguli nchini Jenerali Ulimwengu, ameungana na jopo la mawakili Tundu Lissu, Peter Kibatala na John Malya katika kumtetea Mbowe.Jeneral Ulimwengu alisema haya nje ya Mahakama baada ya maamuzi hayo

“Ombi limekataliwa kwa sababu hatukuwa na kifungu ambacho katika sheria zetu kinafanya kazi katika nchi na maelekezo hayo ni kwamba kwa sababu tuna ‘import’ sheria zetu kutoka Uingereza. Tutafute kifungu ambacho kinaweza kusaidia kuendesha mashtaka, hiyo kazi itafanyika kati ya leo au kesho kwa sababu kesi ya msingi bado ipo na itasikilizwa March 8.” alisema Jenerali Ulimwengu.

Naye Mweneyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe baada ya maaamuzi hayo ya Mahakama alisema jopo la mawakili litahamia mjini Arusha kwenye kesi inayomkabili Mbunge wa Arusha mjini (CHADEMA) Godbless Lema.

Zinazohusiana

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Check Also

Close