M-Pesa na Tigo Pesa Zapokea Uthibitisho Kutoka GSMA


Huduma za kutuma na kupokea pesa kwa njia ya simu zimekuwa na msaada mkubwa kwa watanzania. Huduma za kutuma na kupokea pesa za Tigo Pesa na M-Pesa ni huduma maarufu zaidi na zimekua zikiongoza kwa muda mrefu kwa hapa Tanzania.

Umaarufu na ubora wa huduma za kutuma na kupokea pesa za Tigo Pesa na M-Pesa na sababu nyingine ndio zilizofanya kampuni za Tigo Tanzania (Millicom Group) na Vodacom Tanzania kupokpesujulikanao kama ‘GSMA Mobile Money Certification’. Uthibitisho huo maana yake ni kuwa kampuni hizo zimeweza kutoa huduma salama, kwa uwazi, na kiuthabiti kwa kusimamia haki za wateja na kuzuia miamala ya kihalifu.


GSMA Mobile Money Certification’ ni mkakati wa kimataifa unaolenga kuleta huduma za kifedha salama, wazi na thabiti zaidi kwa mamilioni ya watumiaji wa huduma za kifedha kwa simu za mkononi duniani kote.


Huku kukiwa na zaidi ya akaunti 690 milioni za fedha kwa simu za mkononi duniani, sekta ya simu za mkononi inaboresha maisha duniani na imewezesha mamilioni ya watu wasiokuwa na akaunti za benki kufikiwa na huduma rasmi za kifedha.

Kwa mujibu wa tovuti ya Tigo, GSMA imebainisha kuwa vigezo vinavyotumika kutoa uthibitisho huu vinazingatia viwango vya ubora wa kimataifa katika utoaji huduma za kifedha. Kabla ya kupokea uthibitisho huo, kila mtoa huduma wa fedha kwa njia ya simu za mkononi sharti afikie asilimia 100% ya vigezo vilivyowekwa. Watoa huduma wanaopokea uthibitisho huu ni wale tu waliofanikiwa kuonesha kuwa hatua za uendeshaji wa biashara zao ni miongoni mwa zile zilizo bora, zinazoaminika na kuwajibika zaidi katika mfumo mzima wa utoaji huduma za kifedha duniani.

Watoa huduma za kifedha wengine waliopewa uthibitisho na GSMA Mobile Money Certification ni pamoja na;

  1. Orange Côte d’Ivoire
  2. Safaricom (Kenya),
  3. Telenor Microfinance Bank Ltd. (Easypaisa Pakistan),
  4. Tigo Tanzania (Millicom Group) na
  5. Vodacom Tanzania

Hivi karibuni Safaricom ya Kenya ilitangaza ujio wa huduma ya kutuma na kupokea pesa kupitia PayPal na kuja kwenye huduma za M-Pesa, ikiwa pamoja na huduma ya kuwawezesha watumiaji wa Android kuweza kulipia App kwa kutumia M-pesa.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA