Home Nyingine [Lyrics] Nash Mc Ft. Mau – Shujaa

[Lyrics] Nash Mc Ft. Mau – Shujaa

0
0

Ubeti wa 1
Tumejiuliza sana utarudi siku gani/
Shujaa tuliekutuma kwenye uwanja wa medani/
Uwakomboe ndugu zetu waliotekwa vitani/
Silaha begani, uwanjani,ulimwaga njugu nasikia kama hayawani /
Hazikupita dakika wakapotea hewani/
Wapinzani wakatia mpira kwapani/
Vita ilikua kali msiambiwe si utani/
Tunamshukuru Mungu umerejea nyumbani/
Na furaha isiyo kifani/ naona wafuasi wamejipanga njiani/
Kumpokea mkombozi aliebaki kwenye imani/
Ambae anajua, anapotoka jinsi gani/
Watu wamechoka maisha ni taabani/
Mawazo kichwani,nalia ukame nyumbani/
Ukisema milo mitatu utaulizwa ndio kitu gani?/ Kibwagizo – Mau
Shujaa ndio amefika na ameshinda vita
Nami nawaalika,kumpokea Shujaa
Shujaa aaaaaaaaaah! ×2

Ubeti wa 2
Hakuna alietegemea kama ungerejea/
Hasa kipindi hiki ambacho mengi yametokea/
Achana na maneno wapumbavu wanayoongea/
Kwa vita uliyopigana tulidhani ungedondoka/
Kwa ushindi wako huu, nakuongezea nyota/
Kweli umedhihirisha we ni mzizi usieng’oka/ Shujaa wa kuogopwa/
Umetuacha kwenye dhiki toka ulivyoondoka/
Wachezaji hoi,yani awamu hii chama langu halina kocha/
Benchi lake la ufundi kila mmoja anaropoka/
Nani wa kuyasema na wenzio wanaogopa/
Kambini washatoroka /
Shujaa tunakuamini sauti ya wanyonge ni wewe/
Paza sauti yako wala uchumi wakuelewe, silaha upewe/
Tetea kwenye elimu Kwani uozo ndio kibao/
Wanatutia ujinga wasome watoto wao/

(0)

LEAVE YOUR COMMENT

Your email address will not be published. Required fields are marked *