Nyingine

Lugumi na ufisadi hakuna vifaa vilivyofungwa ila imelipwa mabilioni ya fedha

Ripoti ya mkaguzi na mdhibiti mkuu wa serikali imetaja kuna dalili za ufisadi wa kampuni ya Lugumi katika wizara ya mambo ya ndani kutokana na manunuzi ya ‘E-migration system’ kwa ajili ya idara ya uhamiaji.

“Mzabuni, Lugumi Enterprisiesa Limited, aliwasilisha Makabrasha mawili tofauti ya zabuni yenye bei tofauti ya 37,163,940,127.70 na 39,518,133,666.30; hivyo kushindwa kuthithibitika kwakabrasha sahihi kati ya hayo mawili.

Wajumbe wawili wa kamati ya tathmini hawakutia saini ripoti ya tathmini wala kujaza fomu za agano kinyume na Kifungu cha 37(6) cha PPA, 2011 Kamati ya tathmini ilishindwa kubaini makosa yaliyowasilishwa na Mzabuni Lugumi Enterprises. Hatua hii ilisababisha iliyopelekea Bodi ya Zabuni kuidhinisha bei ambayo haikuwa halisi hivyo kusababisha mabadiliko ya gharama za mkataba kutoka Sh. 37,163,940,127 kwenda Sh 41,475,728,579.50.

Mzabuni Lugumi Enterprises alishindwa kufunga AFIS katika vituo 36 kati ya 152. Mkataba kati ya Lugumi na Wizara ulikuwa na baadhi ya vitu vyenye mchanganuo/vipengele sawa lakini vya bei tofauti hatua iliyopeleka hasara ya Sh. 656,779,032 Jumla ya Sh.1,028,918,464 zililipwa kama gharama ya Mafunzo lakini mafunzo hayo hayakufanyika. Jumla ya Sh.3,304,000,000 zililipwa kama gharama za Matengenezo lakini matengenezo hayo hayakufanyika.

Hapakuwa na uthibitisho kuwa Mzabuni alilipa kodi kwa TRA yenye thamani ya Sh. 2,250,917,455 kati ya Shs. 5,757,393,509.60 zilizopaswa kulipwa licha ya Mzabuni kupata msamaha wa Kodi toka TRA wa Sh.3, 506, 476,054.50 katika mkataba wa Shs. 37,742,913,007.35. Baadhi ya gharama ya vifaa kwenye Mkataba ilikuwa juu ya bei ya soko hali iliyosababisha hasara ya jumla ya Shs. 5,964,112,462.

SOMA NA HII:  Marufuku Matumizi ya Takwimu za Kampuni ya Geopoll - Dkt. Mwakyembe

Zinazohusiana

Leave a Reply

Your email address will not be published.