Nyingine

List Ya Michezo ya Wanyama Ambayo Inawezekana Hujawahi Kuisikia

Linapokuja suala la michezo inayowashirikisha wanyama, jambo linakuja akilini mwa watu wengi ni mbio za farasi ,mapambano ya kuku na nk . Hata hivyo, kama unahitaji msisimko zaidi katika maisha yako, sisi tupo hapa kuonyesha jinsi wanyama mbalimbali wanavyotumika kwenye michezo sehemu mbalimbali duniani.

Nani anajua, pengine baada ya kuona list hii, utapata shujaa mpya wa michezo miongoni mwa …WANYAMA.

Mashindano ya Sungura kuruka vikwazo.

Kwanza kwenye orodha yetu – pengine huu ndio mchezo mzuri zaidi kugunduliwa – mashindano ya kuruka yanayo husisha sungura. Tunaamini mashindano ya kuruka ya farasi yamechangia kuibuka kwa mchezo huu, hapa kunakuwa na aina tofauti za sungura zikirukaruka vikwazo katika sehemu ndogo.

Mchezo huu asili yake ni Sweden na umeenea Uingereza na Marekani.

Kutema Panzi

Sheria ya mchezo wa kutema panzi ni rahisi: unachukua panzi aliyekufa, na kuweka mdomoni mwako kisha unamrusha mbali kwa kutumia mate yako kama unaweza. Mshiriki ambaye ataweza kumrusha panzi mbali zaidi kwa kutumia mate yake anakuwa mshindi.

Mchezo huu ulianzishwa na entomologist Tom Turpin katika Chuo Kikuu cha Purdue. Tangu wakati huo, mchezo huu unachezwa katika vyuo vikuu vingine na kwenye matukio mbalimbali.

 

Mbio za Konokono

Mbio za konokono …….polepole. Katika mchezo huu pekee, konokono wawili au zaidi wanakimbia kwenye eneo lenye mviringo wenye inchi 13-14. Ili kutofautisha kila mshishiriki, wanaandika namba ya mashindano juu ya konokono au kuambatanisha stika ndogo.

SOMA NA HII:  Swali la Siku: - Kati ya Vitu Hivi 3, Ni Kitu Gani Ni Ngumu Kwako Kuishi Bila Kukifanya?

Kuna matukio mbalimbali ya mbio za konokono yanayofanyika duniani kote kila mwaka lakini  “Annual World Snail Racing Championships” ya Nchini Uingereza ni maarufu zaidi.

Mpira wa kikapu unaochezwa na Tembo

Pengine hii ni moja ya sababu kuu itakayofanya utamani kutembelea Thailand. Tembo wanapata mafunzo ya kucheza mpira wa kikapu kama sehemu ya ubunifu wa serikali ili kuboresha afya zao. Mafunzo huanza na masomo ya ujuzi wa kawaida wa kumiliki mpira. Kisha walinzi hufundisha tembo jinsi ya kusimama kwa miguu yao ya nyuma, kutembea na mpira na hatimaye kufunga goli kwa kutumia mkonge wake .

Inatakiwa kufanya kazi kwa bidii kutoa mafunzo kwa tembo lakini ina thamani yake, show yake ni ya kuvutia sana.

Mbwa kucheza na mawimbi ya bahari

Mchezo huu unaanza kupata umaarufu pia. Kama unapendo mbwa na kucheza baharini, na unaweza kumfundisha mbwa wako kusimama wima kwenye bodi wakati mawimbi yanapiga, basi mchezo huu ni kwa ajili yako.

Mchezo ulianza kuchezwa katika jiji la San Diego, na limekuwa jambo kubwa katika nchi ya Australia pia.

Olympics ya Nguruwe

Mchezo huu pengine ni moja ya matukio yanavutia zaidi. Olympic ya nguruwe inashindanisha nguruwe ‘wanamichezo’ katika kuogelea, kukimbia , na hata kuwagawa katika timu kutafuta mpira wa soka uliopo katika eneo lenye mafuta ya samaki. Na tuna kuisthakikishia kuwa nguruwe hawa hawataishia kwenye meza ya chakula cha jioni. Bali huachwa kwa lengo la kuzalisha kizazi kipya cha nguruwe wanamichezo.

SOMA NA HII:  Teknolojia 5 Maarufu kwenye Magari Kwa Sasa

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako