“LG Smart Fridge” Itakukumbusha lini chakula chako kinaisha muda wake


Mwaka jana, Samsung iliunganisha tablet kubwa mbele ya friji na wakaiita “fridge smart”. Watu waliinunua, na kulikuwa na malalamiko mengi. Mwaka huu Samsung inatumaini kuwa baadhi ya sasisho za programu kwenye teknolojia ya friji hiyo zitaiboresha zaidi. Lakini haitakuwa hivyo. Badala yake, Samsung smart fridge bado itasuasua kwenye soko. Kwa sababu LG imeipiga kikumbo Samsung kwa kutengeneza friji za Windows.

Smart Instaview Friji kutoka LG ni friji erevu (smart fridge) ya kwanza kutengenezwa na kampuni hiyo, na imekuwa bora zaidi, imetengeneza katika matoleo mawili tofauti: moja ikiwa na Alexa voice control na WebOS, na nyingine ina Cortana voice control na Windows 10. Friji hizi zinaonekana zinatumia Intel Atom processor.

Kwa sababu zinatumia mifumo tofauti ya uendeshaji (operating systems) ufanyaji kazi pia ni tofauti kati ya friji hizi mbili.

Pamoja na tofauti inayoonekana katika ufanyaji kazi, muonekana wa skrini ya msingi kwa kila friji unafanana sana. Ni bodi nyeupe ya kawaida inayokuwezesha kuweka taarifa ya vitu inavyotakiwa kukukumbusha, tarehe za kumalizika kwa bidhaa (expiration dates), maelezo, na muda ambao huhesabu katika mfumo wa wakati halisi.

Unapokuwa hujaridhika na kioo cheusi, unaweza kuweka kiwe cha kawaida ili uweze kuona vitu vilivyomo ndani . Pia kuna kamera ya ndani ili uweze kuona ndani ya friji bila ya kuifungua.

LG inatarajia kuzindua friji hii baadaye mwaka huu, lakini mpaka sasa hakuna taarifa juu ya bei au upatikanaji wa bidhaa hii.

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *