Sambaza:

Leo ni siku ya Malaria duniani. Tanzania na nchi nyingine za Afrika zimeendelea kupamba na ugonjwa huu wakati chanjo yake ikiendelea kufanyiwa majaribio.

Nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya kongo, changa moto bado ni kubwa katika kuutokomeza ugonjwa huo kama ambavyo malengo ya shirika la afya duniani WHO lilivyo la kumaliza ungojwa huo mpaka ifikapo mwaka 2030 zaidi ya asilimia arobaini ya raia wa DRC wamefariki dunia kutokana na ugonjwa wa malaria na pia Congo na Nigeria zimekuwa nchi za kwanza duniani kuathiriwa na ugonjwa huo.

Chanjo ya kwanza ya malaria duniani itajaribiwa kwa kiwango kikubwa katika nchi ya Ghana, Kenya na Malawi kuanzia mwaka ujao.

SOMA NA HII:  Hali ni mbaya sana kwa tovuti za Pirates na wazee wa Torrent

Shirika la Afya Duniani WHO limesema chanjo hizo zinaweza kuokoa maisha ya maelfu ya maisha, huku malari ikiendelea kupoteza maisha ya watu.

Mpango huo ambao uko katika majaribio utahusisha zaidi ya watoto 700,000 wenye umri kati ya miezi mitano na mwaka mmoja na nusu.

Haijathibitika kwamba chanjo hiyo inaweza kufanya kazi kwa asilimia mia moja, lakini wataalamu wa masuala ya afya wanasema chanjo hiyo ni hatua muhimu katika mapambano ya dunia dhidi ya ugonjwa wa malaria.

Hii inafuata miongo kadhaa ya tafiti ya kutafuta ugonjwa ambao unaongoza kwa vifo duniani.

SOMA NA HII:  Teknolojia 5 Maarufu kwenye Magari Kwa Sasa

Chanjo hiyo mpya, itakwenda sambamba na hatua nyengine za kujikinga kama vile neti, dawa za kufukuza mbu, na dawa za kukinga malaria.

Wakati wa majaribio, maelfu ya watoto watapewa chanjo hiyo mara nne katika kipindi cha miaka miwili.

Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako