Sambaza:

1. Aprili 6, 1994- Rwanda iliingia kwenye mauaji na maovu makubwa.

Mauaji ya Kimbari ya Rwanda yalikuwa mauaji ya halaiki nchini Rwanda mnamo mwaka wa 1994 ambapo Watutsi, Watwa na baadhi ya watu wa kabila la Kihutu waliuliwa na serikali iliyosimamiwa na viongozi wa Kihutu.

 

Katika kipindi cha takriban siku 100, kuanzia kuuliwa kwa hayati Rais Juvenal Habyarmana na mwenzake wa Burundi Cyprien Ntaryamira tarehe 6 Aprili hadi katikati mwa mwezi Julai, walau watu 500,000 waliuawa, au karibu asilimia 20% ya idadi ya watu nchini Rwanda wakati huo.

Kuuawa Habyarimana tarehe 6 Aprili 1994 kulikuwa chanzo muhimu cha mauaji ya kimbari nchini humo. Kuhusiana na kuuawa Habyarimana, Wahutu wenye misimamo ya mkali walihusisha tukio la kutunguliwa ndege yake na wapinzani wa Kitutsi na kulitumia kama kisingizio cha kuanzishia mashambulio na mauaji makubwa na ya kutisha dhidi ya Watutsi, Watwa na Wahutu wenye misimamo ya wastani.

SOMA NA HII:  Swali la Siku: - Kati ya Vitu Hivi 3, Ni Kitu Gani Ni Ngumu Kwako Kuishi Bila Kukifanya?

Rais Paul Kagame ametuhumu Ufaransa kwa kuhusika na mauaji hayo ingawa Ufaransa imekanusha vikali madai hayo.

2. Michezo ya Olimpiki ya Kisasa ilianza mjini Athens (Ugiriki).

Michezo ya Olimpiki ya Kale ilifanyika tangu tarehe isiyojulikana lakini kwa uhakika kuanzia mwaka 776 KK hadi mwaka 393 BK katika mtaa Olimpia nchini Ugiriki.

 

Waanzilishi wake walijizatiti kwa miungu wa Kiolimpiki na walivuka kipindi cha kale katika maeneo ya Olimpia. Waliendelea kwa karibu karne 12, mpaka pale Mfalme Theodosius alipotoa amri mwaka 393 baada ya kuzaliwa kwa Kristo kuwa wasiokua na dini wapigwe marufuku .

Michezo ya Olimpiki ya Kisasa ya kwanza ilitokea Aprili 6, mwaka 1896 mjini Athens (Ugiriki). Mwanzilishi alikuwa Mfaransa Pierre de Coubertin aliyetaka kutumia kielelezo cha michezo ya kale kwa kujenga uhusiano mzuri kati ya vijana wa nchi mbalimbali na kuwapatia nafasi ya kushindana kwenye uwanja wa michezo badala ya uwanja wa vita. Coubertin alianzisha Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (International Olympic Committee – IOC).

SOMA NA HII:  Hali ni mbaya sana kwa tovuti za Pirates na wazee wa Torrent

Michezo hii ya kisasa imeendelea kila baada ya miaka minne isipokuwa 1916, 1940 na 1944 kwa sababu ya Vita Kuu ya Kwanza na ya Pili ya Dunia.

Michezo ya kisasa hufanyika katika mji tofauti kila safari. Michezo ya 2004 ilifanyika Athens, ya 2008 huko Beijing na ya 2012 London.

3. Animation cartoon ya kwanza ilipata hatimiliki 6 Aprili, 1906

“Humorous Phases of Funny Faces” kutoka kwa J. Stuart Blackton ilitolewa 1906. Inaonyesha mchora katuni akichora nyuso kwenye ubao, mpaka sasa wanahistoria wa filamu wanaamini hii ndo animation film ya kwanza.

 

SOMA NA HII:  Je una bashiri "kubeti" ili kujikwamua na matatizo ya kimaisha ?

4.  Microsoft ilitangaza kutoa Windows 3.1,ikiwa ni maboresho ya Windows 3.0 (6 Aprili 1992)


Windows 3.1, ilianza kuunzwa rasmi April 1992 kama mbadala wa Windows 3.0. Matoleo mengine yalitolewa kati ya mwaka 1992 na 1994 hadi mfululizo huo ulivyositishwa baada ya kutoka kwa Windows 95. Ndani ya muda wake, Windows 3.1 ilileta maboresho kwenye mfumo ambao bado upo MS-DOS, ikiwemo kuboresha system stability, kupanua msaada kwa ajili ya multimedia, TrueType fonts, na workgroup networking.

5. Ufaransa ilipitisha sheria mpya juu ya ukahaba na kufanya kulipia ngono kuwa haramu (Aprili 6, 2016)

Ufaransa ilipitisha kitendo cha kulipia ngono kuwa haramu baada ya wabunge kupitisha sheria mpya kuhusu ukahaba.

Chini ya sheria mpya , mtu yeyote atakayekamatwa analipia ngono atalipishwa faini na atatakiwa kuhudhuria darasa la madhara ya ukahaba.

Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako