Nyingine

Lema: Mwanangu aliniuliza baba nifanye kosa gani ili nije tuishi wote gerezani

Baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kumuachia kwa dhamana Mbunge wa Arusha Mjini kupitia CHADEMA, Godbless Lema ambaye amesota gerezani kwa zaidi ya miezi minne, kwa mara ya kwanza amezungumza na  kuwashukuru wale waliompigania. Lema amedai anaenda kumuona mwanaye ambaye alitaka kufikia uwamuzi wa kutaka kufanya kosa ili na yeye aingie gerezani kukaa na baba yake.

“Leo nina mambo machache sana ya kuongea, ninamshukuru sana mwenyezi Mungu, mke wangu, familia yangu, mawakili, viongozi wa chama na wananchi wote waliokuwa na mimi. Na kwa namna ya pekee mke wangu, kama ningepata nafasi ya kuoa tena, ningemuoa yeye. Pia mtoto wangu alifikia hatua akasema anatamani kufanya kosa ili aje alale na mimi gerezani, na akauliza ni kosa gani afanye ili aletwe gerezani,” alisema Lema.

Mbunge huyo ameachiwa kwa dhamana yenye masharti ya wadhamini wawili wanaoaminika pamoja na kusaini bondi ya shilingi milioni 1 kila mmoja.

Zinazohusiana

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *