Nyingine

Lameck Ditto: Bongo Flava ni Kiswahili haitopotea leo wala kesho

on

Akiongea kwenye kipindi cha VMix cha Channel 10, Lameck Ditto hitmaker wa Moyo Sukuma Damu amesema muziki wa Bongo Flava utaendelea kudumu milele.

“Bongo Flava ni Kiswahili, moja ya vitu vinavyoweka ladha kwenye muziki wetu wa Bongo Flava ni Kiswahili na Kiswahili bado kipo na kinazidi kukua, kuenea na kusambaa kila kukicha maeneo mbalimbali Afrika Mashariki na duniani kote,”

“Hivyo sioni kama muziki wetu unapungua ladha kama Kiswahili kinazidi kukua na kutumika maeneo mbalimbali kwa maana hiyo Bongo Flava haiwezi kupotea leo wala kesho.

About Benix Matrix

Leave a Reply

Your email address will not be published.