Home Nyingine Lamar: Watayarishaji wa sasa kila mmoja anajiona ni mkubwa

Lamar: Watayarishaji wa sasa kila mmoja anajiona ni mkubwa

0
0

Kupitia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio , Mtayarishaji wa muziki Lamar kutoka Fish Crab amefunguka ya moyoni kuhusu watayarishaji wa muziki wa sasa.

Lamar amesema watayarishaji wa sasa kila mmoja anajiona ni mkubwa wanashindwa kupeana ushirikiano ndio maana hata midundo yao mingi inafanana.

“Producers wa sasa wana kitu wenyewe wanakiita ‘ego’ kiasi kwamba wanashindwa hata kupatiana ushirikiano ndiyo maana ukisikiliza wimbo huu unafanana na ule, hata ule mzuka ambao zamani ukisikiliza nyimbo unapata hakuna, lakini zamani ukisikia wimbo alofanya Majani, Dunga au Master Jay lazima kuna kitu cha tofauti utakipata,” amesema Lamar.

“Zamani Majani mpaka akukubali ufanye naye kazi inabidi uwe na adabu lakini pia uwe na kitu cha pekee cha kumshawishi ndiyo maana hata nilivyoondoka kwake niliweza kufanya kazi na Dunga na waandaji wengine wanne tofauti kitu ambacho kilinipa ujuzi mkubwa kabla ya kuanzisha lebo yangu mwenyewe,” ameongeza.

(0)

LEAVE YOUR COMMENT

Your email address will not be published. Required fields are marked *