Nyingine

Lake oil sasa kuuza mafuta kisasa yaja na mfumo wa kadi

Kampuni ya mafuta ya lake oil imeanzisha mfumo mpya wa kununua mafuta kupitia kadi maalum ambayo inampa nafasi mteja wa kampuni hiyo kujaza mafuta katika vituo vya kampuni hiyo nchi nzima kwa kutumia kadi pesa.

Akizungumzia mfumo huo mkuu wa idara ya mauzo na masoko ya rejareaja nchini Aluw Hamad amesema kwa kipindi chote kampuni hiyo Ilikuwa na changamoto ambazo zilikua zikimnyanyasa mteja na kumfanya asifurahie huduma nchini.

Alisema miongoni mwa matatizo yanayowasumbua wateja wa mafuta nikushindwa kupanga bajeti ya mafuta,lakini mfumo huu mpya wa kadi unamuwezesha mteja kuweka pesa katika kadi yake ya mafuta kwa mwezi hivyo kumrahisishisia mteja kuepuka kuharibu bajeti.

Soma na hizi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Close