Intaneti

Kwaheri Google Instant Search

Unakumbuka unapojaribu kuandika kitu katika sehemu ya utafutaji ya Google na tayari inakuonyesha matokeo ya utafutaji ya nini inadhani unataka kuandika kabla ya kubonyeza enter? Katika ubora wake, ingeweza kuonyesha matokeo yanayotakiwa na katika siku mbaya, ingeweza kuonyesha idadi kubwa ya matokeo ya utafutaji yasiyohusiana na wewe unapo andika neno kwenye sehemu ya kutafuta.

Sasa, Google imepiga bomu kwenye eneo hili. Sababu? Rununu(mobile)!

Google wanadai kwamba “utafutaji mwingi zaidi hutokea kwenye simu, kutokana na uingizaji tofauti, uingiliano na vikwazo vya skrini. Kwa kuzingatia hayo, tumeamua kuondoa Google Instant, ili tuweze kuzingatia zaidi kwenye njia za kufanya Utafutaji kuwa wa kasi na kwa urahisi zaidi kwenye vifaa vyote”

Sasa, usichanganye Utafutaji wa Papo hapo wa Google (Google’s Instant Search) na mapendekezo ya utafutaji (search suggestions) ambayo huonekana chini ya sanduku la utafutaji. Maonyesho ya kwanza ya matokeo ya utafutaji wakati unapoandika na kabla ya kubonyeza icon ya ‘Tafuta’ au kubonyeza ‘Enter’. Wakati mapendekezo ya utafutaji (search suggestions) yanaonekana kwa kushuka chini na yanategemea utafutaji wako wa zamani na vitu ambavyo watu wengine wanatafuta – hii bado ipo, asante Mungu.

Kwa hiyo, uhakikisho wa utafutaji wa papo kwa hapo (Instant search), hauta kumbukwa sana.

Nadhani kitu kingine ambacho Google inapaswa kufuta ni kitufe cha “I’m feeling lucky”.

SOMA NA HII:  👌🏾: Je, unajua Sasa Unaweza Kutuma Ujumbe wa Sauti kwenye Whatsapp Kutumia Ok Google?

Mada zinazohusiana

Zinazohusiana

Leave a Reply

Your email address will not be published.