Habari za Teknolojia

Kwa Mujibu Wa LaptopMag, Apple Sio Brand Namba Moja Tena

Wapenzi wa Windows hivi sasa:

Kila mtu anajua (ooh, sio kila mtu) kuwa moja ya sababu kubwa ya watu kununua MacBook ni kwa faida ya maisha na nguvu ya brand ya Apple. Naam, swala hili karibuni litakuwa ni historia, taarifa zilizotolewa na LaptopMag, Apple imeshuka, hawapo tena kwenye nafasi ya kwanza (Ambayo wameishikilia tangu mwaka 2013) na, sasa wapo, # 5.

Ili kufika katika nafasi za juu, LaptopMag inatumia vigezo mbalimbali kama  utendaji wa bidhaa  katika maeneo kama msaada kwa wateja, ubunifu, ubora, na bei. Pia wamethibitisha takwimu zao kwa kuonyesha utendaji wa wastani wa Macbooks , ambao si sawa na bei yake.

Kwa sasa list inaongozwa na Lenovo ikifatiwa na Asus, Dell, na HP.

Mmmmh, si ni kejeli kusema Acer na Apple wamefungana katika nafasi ya tano?

SOMA NA HII:  SUA kuokoa asilimia 40 ya mazao yanayoharibiwa na panya shambani

Zinazohusiana

TOA MAONI

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako