Sambaza:

Kwa mara ya pili mfululizo Tanzania imechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Kituo cha Madini na Kijiosayansi cha Afrika (AMGC).

Wajumbe mbalimbali wa Mkutano wa Baraza la Uongozi wa AMGC wakiwa katika kikao cha 37 nchini Tanzania.

Tanzania imechaguliwa tarehe 15 Septemba, 2017 wakati wa kuhitimishwa kwa Mkutano wa 37 wa Baraza hilo uliofanyika katika Kituo cha AMGC, kilichopo Kunduchi jijini Dar es Salaam.

Mkutano wa Baraza la Uongozi la Kituo hicho ulitanguliwa na mkutano wa Wajumbe wa Bodi ya AMGC na baadaye kufuatiwa na mkutano wa Makatibu Wakuu kutoka nchi wanachama wa kituo husika.

Balozi wa Msumbiji Nchini Tanzania, Monica Patricio Clemente akichangia hoja katika Mkutano wa Baraza la Uongozi wa AMGC jijini Dar es salaam.

Wakati wa kuhitimishwa kwa mkutano husika, Wajumbe wameazimia utekelezwaji wa masuala kadhaa miongoni mwa nchi wanachama ikiwemo kulipa ada za uanachama, nchi wanachama kukitumia ipasavyo kituo hicho na kutafuta wateja kwa ajili ya kutumia huduma zinazotolewa na kituo hicho na kuhamasisha na kujikita katika shughuli za uongezaji thamani madini.

Aidha, maazimio mengine yaliyopendekezwa ni pamoja na; kusisitiza masuala ya uongezaji thamani madini miongoni mwa nchi wanachama. Aidha, pamoja na maazimio hayo, nchi wanachama wamepokea taarifa ya kikao cha 37 kilichopita.

Mwakilishi Mkazi wa Masuala ya Uchumi kutoka Ubalozi wa China, Lin Zhiyong mmoja wa wafadhili wa AMGC akikabidhi zawadi kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kituo, Ibrahim Shaddad kwa ushirikiano mwema uliopo kati yao.t

Akizungumza wakati wa kufunga mkutano huo, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Prof. James Mdoe amewakumbusha nchi wanachama kuzingatia maelekezo yaliyotolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo. Waziri Mkuu Majaliwa aliwata wanachama wa AMGC kulipa ada ya uanachama, kuhakikisha kuwa kituo hicho kinapewa idhibati na kukitumia kituo huska kwa ajili ya shughuli za uongezaji thamani madini.

SOMA NA HII:  Ukosefu wa Ajira Wasababisha Website ya Chuo Tanzania Kudukuliwa

Wanachama wa mkutano husika wameweka maadhimio ya mkutano wa 38 kufanyika nchini Sudani Kaskazini huku Tanzania ikiwa ni Mwenyekiti wa mkutano huo.

Nchi wanachama wa kituo cha AMGC ni Tanzania, Angola, Msumbiji, Sudani Kaskazini, Ethiopia, Uganda, Kenya, Comoro na Kenya. Aidha, nchi ya Burundi imeshukuru kuwa mgeni mwalikwa katika kikao hicho na kuahidi kuwa mmoja wa wanachama wa kituo hicho.


Sambaza:

Written by Mediahuru

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili.

Leave a Comment

Kumbuka Ni Muhimu Kuandika Jina Lako