Jinsi ya Kuzuia Kuibiwa Vifaa Vya Ndani Vya Kompyuta Yako


Kwanza kabisa unatakiwa ufahamu kuwa sio rahisi kuweza kufahamu kila kifaa cha kompyuta yako kilicho ndani, lakini hapa ninakuwezesha kufanya hivyo kwa njia nyepesi kabisa.

Leo nimekuletea programu maalum kabisa kwa ajili ya kuorodhesha kila kilichomo ndani ya kompyuta yako, kwa majina pamoja na Model zake, hivyo basi unaweza kuvirekodi pembeni hata katika Diary yako kwa usalama zaidi, ili ikitokea umetofautiana na fundi wako basi unafungua programu yako na kisha unaiomba ikuorodheshee vifaa vya kompyuta yako na hapo utaweza kucompare kama ni vilevile ulivyovirekodi mwanzo au sivyo, na mwisho kabisa utafahamu ukweli uko wapi.

Uzuri wa programu hii ni kwamba;

 1. Haina saizi kubwa
 2. Ni rahisi kutumia
 3. Haina mambo mengi wakati wa kuinstall

Zifuatazo ni hatua za kuinstall:

 1. Download programu hii kwa kubonyeza hapa
 2. Kisha install kama kawaida
 3. Ukimaliza kuinstall nenda kwenye desktop kisha itafute utaona imeandikwa “Speccy”
 4. Double click/bonyeza mara 2 ili kuifungua.

Ikifunguka programu hii itakuwa na muonekano kama inavyoonekana hapa chini:

Hapo unaweza kuona mwenyewe vitu gani vimeorodheshwa kwa majina, saizi pamoja na modeli zake, kwa mfano;

 • CPU/PROCESSOR/ (UBONGO WA COMPUTER)
 • RAM/ (VITUNZIO VYA DATA KWA MUDA ZINAOTUMIKA)
 • MOTHERBOARD/ (KIFAA KINACHOUNGANISHA VITU VYOTE NDANI YA COMPUTER)
 • STORAGE/HARD DISK/ (KIFAA KINACHOTUNZA DATA ZAKO ZOTE)
 • N.K

Wengi wetu huibiwa RAM, HDD, MOTHERBOARD na PROCESSOR, hivyo basi unatakiwa kufahamu vitu vidogo kama hivi ili kuepusha matatizo na mtu, na sio lazima awe fundi tu, wapo hata marafiki wasio waaminifu ambao tunawaazima kompyuta lakini zinarudi zimebadilishwa vitu.

Kwa Habari Zaidi Na Maujanja Mbalimbali Ya Teknolojia Endelea Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Wa Mediahuru Kila Siku Kwani Daima Tunaaminika Katika Teknolojia!

 

0 Comments

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ZINAZOHUSIANA